Nenda kwa yaliyomo

Klorpropamidi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Klorpropamidi (Chlorpropamide), inayouzwa kwa jina la chapa Diabinese miongoni mwa zingine, ni dawa inayotumika kutibu kisukari cha aina ya 2.[1] Inatumika pamoja na utaratibu maalumu wa lishe na mazoezi [1] na ni matibabu ya mstari wa pili.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maumivu ya kichwa, kizunguzungu, kufa ganzi, kuhisi usumbufu tumboni, kuongeza uzito na kichefuchefu.[2][1] Madhara yake mengine yanaweza kujumuisha sukari ya chini ya damu na matatizo ya ini.[2][1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Ni sulfonylurea ya kizazi cha kwanza na hufanya kazi kwa kuongeza kutolewa kwa insulini.[1][2][3]

Klorpropamidi iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1958.[1] Uuzaji wake wa kibiashara umekatishwa nchini Marekani.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 1.8 "Chlorpropamide Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 4 Machi 2021. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 2.2 "Sulfonylureas, First Generation". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 Januari 2022. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 749. ISBN 978-0857114105.
  4. "Drugs@FDA: FDA-Approved Drugs". www.accessdata.fda.gov. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 Machi 2016. Iliwekwa mnamo 4 Januari 2022.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Klorpropamidi kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.