Kinanda cha filimbi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kinanda cha filimbi huko Kanisa la Moravian Mamre, Afrika Kusini
Carol Williams akipiga kwenye kinanda kikubwa cha filimbi kwenye kanisa la Chuo cha Kijeshi cha Westpoint, Marekani

Kinanda cha filimbi (ing. pipe organ) ni ala ya muziki inayotoa sauti kwa njia ya kupuliza hewa kupitia filimbi zinazochaguliwa kwa njia ya kupiga vibao vya kinanda kwa vidole vya mkono au -kwenye kinanda cha filimbi kikubwa zaida- pia kwa miguu.

Filimbi hupangwa kwa safu zenye sauti za kufanana. Kwa kawaida kinanda cha filimbi huwa na safu kadhaa za filimbi kama ni kikubwa hata makumi. Kila filimbi kwenye safu yake ina kiimbo chake. Mpiga kinanda anaweza kuunganisha safu mbalimbali na kwa kupiga kibao kinacholingana na kiimbo fulani kiimbo hiki kinatolewa kwenye sauti mbalimbali kwa wakati mojs.

Asili ya mwendo wa hewa ilikuwa viriba vilivyokanagwa na msaidizi, siku hizi kuna injini ya umeme inayosukuma hewa katika kinanda. Kwa kupiga kibao valvu inafunguliwa inayopeleka hewa kwa filimbi za safu zilizochaguliwa na mwanamuziki.

Kinanda sahili huwa na seti moja ya vibao, mara nyingi pamoja na seti ya ziadi kwa matumizi ya miguu. Vinanda vikubwa zaidi huwa na seti hadi nne za mikono na viwili vya miguu pamoja na safu nyingi za filimbi.

Taarifa za kwanza kuhusu matumizi ya vinanda zilihifadhifa kati ya Wagiriki wa Kale na baadaye na Waroma. Tangu karne ya 8 BK kunataarifa ya kwanza kuhusu vinanda katika makanisa. Ala hii iliendelea kuboreshwa polepole katika mwendo wa karne nyingi hasa katika Ulaya ya Magharibi na Kati. Tangu karne ya 18 ala hizo zilikomaa na muziki iliyoandikwa wakati ule inatumiwa hadi leo.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons

Mkusanyo wa data[hariri | hariri chanzo]

Video za vinanda vya filimbi[hariri | hariri chanzo]