Kilotani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kilotani ni kipimo kinachotaja tani 1,000.

Tani ni kipimo cha SI cha masi.

Mara nyingi hutumiwa kwa kutaja nguvu ya mlipuko wa bomu la nyuklia. Bomu la kwanza la aina hii lililipuka tarehe 16 Julai 1945 karibu na Los Alamos (Marekani likawa jaribio kwa matumizi ya kwanza ya nishati ya nyuklia ya kijeshi yaliyofuata kwenye mashambuluio ya Marekani dhidi ya Japani mjini Hiroshima tarehe 6 Agosti 1945. Bomu la Los Alamos ilikuwa na nguvu ya mlipuko wa tani 20,000 za kilipukaji cha TNT (=kilotani 20), na nguvu ya bomu la Hiroshima lililingana na tani 13,000 za TNT (kilotani 13).

Kuanzia kilotani 1,000 kipimo cha megatani kimekuwa kawaida.