Kiido

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bandera ya Kiido

Kiido ni lugha ya kupangwa. Inafanana sana na Kiesperanto, lakini haizungumzwi na watu wengi kama Kiesperanto.

Serufi[hariri | hariri chanzo]

Nomino (majina) zote zinahitimu kwa kiambishi tawali -o, kwa mfano "arbo" (mti). Wingi wa nomino unahitimu kwa -i (arbi = miti).

Vivumishi vinahitimu kwa kiambishi tawali -a, kwa mfano "alta" (-refu).

Vitenzi vina viambishi tamati mbalimbali:

  • -ar inatumika kwa vitenzi-jina (kwa mfano "facar" = "kufanya")
  • -as inatumika kwa njeo ya wakati uliopo (kwa mfano "me facas" = "ninafanya"
  • -is inatumika kwa njeo ya wakati uliopita (kwa mfano "me facis" = "nilifanya" au "nimefanya")
  • -os inatumika kwa njeo ya wakati ujao (kwa mfano "me facos" = "nitafanya")
  • -us inatumika kwa hali a masharti (kwa mfano "me facus" = "ningefanya")
  • -ez inatumika kwa hali ya kuamuru (kwa mfano "facez!" = "fanya!"; "il facez" = "afanye")

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiido kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.