Kigezo:Kamatimu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

kamatimu ni jina katika Agikuyu la wanaume ambao baado hawajajiunga na jamii ya wazee,Kigezo:"adhuri".Sherehe maarufu ya "Mburi ya Kiama" huwa fursa ya Kamatimu kuoredheshwa kama mzee. Katika sherehe hizi mbuzi wawili huchinjwa kama ishara ya ombi na kafara kwa niaba ya Kamatimu. Sherehe hii ni maarufu eneo la mkoa wa katikati na haswa hufanyika mahala ambako kuna msitu. Hii ni baadhi ya tamaduni chache zilizohifadhiwa.


Kwa kawaida kamatimu anaweza kujiunga na wengine kwenye sherehe lakini kuna mengi asiyoweza kuyafanya. mojawapo ya haya ni, hana uwezo wa kushirikishwa kwenye kikao cha kutoa maamuzi yanayohusiana na jamii.