Nenda kwa yaliyomo

Kigezo:Databox

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kigezo:Databox
kigezo cha Wikimedia

Main documentation is maintained at Wikidata:Template:Databox/doc

Moduli hii hutoa mfumo rahisi sana wa sanduku la maelezo (infobox) kulingana na data kutoka Wikidata. Inafanya kazi yenyewe (automated), haihitaji usanidi wowote ili kutumika, na haina mabadiliko kulingana na aina ya kipengele (mtu, mahali...).

Inafanyaje kazi?

[hariri chanzo]

Moduli hii ndiyo msimbo wa nyuma (backend code) wa Kigezo cha Databox.

Inatumia kipengele cha Wikidata kilichounganishwa na ukurasa wa sasa au kipengele ambacho ID yake imejazwa kwenye kigezo cha item ili kutengeneza infobox yenyewe.

Algorithm yake ya msingi ni:

  • Kutumia lebo ya kipengele au, ikiwa haipo, jina la ukurasa kwa ajili ya kichwa cha infobox.
  • Kutumia thamani ya P18 kwa ajili ya picha kuu.
  • Kutumia thamani za P31 kwa ajili ya kichwa cha jedwali la data.
  • Kuchukua sifa (properties) zote zinazotumiwa na kipengele hicho, kuzipanga kulingana na MediaWiki:Wikibase-SortedProperties, na kwa kila moja:
    • Ikiwa sifa ina aina ya data ya external-id, commonsMedia au quantity, haitaonyesha chochote.
    • Ikiwa sifa ipo kwenye mpangilio wa site_excluded_properties wa moduli, haitaonyesha chochote (hii hufanyika ili kuchuja sifa zisizo na umuhimu sana katika infobox).
    • Ikiwa sifa ina zaidi ya thamani 5, haitaonyesha chochote (ili kuepuka orodha ndefu kwenye infobox).
    • Inatumia mfumo wa kawaida wa Wikibase kuonyesha thamani zenye daraja "bora" (i.e. thamani zenye daraja la "preferred", zikiwepo, na kama hazipo, zile zenye daraja la "normal").
  • Ikiwa kuna thamani ya P625, basi itaonyesha ramani kwa kutumia Kartographer.


Rahisi kutumia

[hariri chanzo]

Hakikisha msimbo wa Moduli umewekwa
1. Databox inatumia msimbo wa Lua. Msimbo huo utaongezwa kwenye ukurasa wa Module:Databox.

  • Unganisha ukurasa mpya wa Wikipedia ulioundwa (Module:Databox) na kipengele cha Wikidata cha Module:Databox (Q53931871)

Hakikisha msimbo wa Kigezo umewekwa
2. Ili kuitisha kigezo cha databox, hakikisha msimbo wa kigezo hapa chini umeongezwa kwenye ukurasa wa Template:Databox:

{{#invoke:Databox|databox|useImage={{{useImage|}}}|excludeProperties={{{excludeProperties|}}}}}
  • Unganisha ukurasa mpya wa Template:Databox na kipengele cha Wikidata cha Template:Databox (Q20702632)

Uko tayari kuongeza databoxes kwenye kurasa zako za Wikipedia
3. Nenda kwenye ukurasa au makala unayotaka kuongeza databox, ingia kwenye hali ya kuhariri (edit mode) na uongeze kigezo cha {{Databox}} juu kabisa ya ukurasa.

4. Hakiki ukurasa ili kuhakikisha databox imeonekana, na kisha chapisha (publish) ili kuhifadhi mabadiliko yako.


Kuhariri data ya Databox

[hariri chanzo]

Wakati mwingine data inaweza kuwa na makosa au imepitwa na wakati na inahitaji kubadilishwa au kuhuishwa, lakini huwezi kufanya hivyo kutoka kwenye ukurasa wa sasa. Data inayoonekana kwenye databox haihifadhiwi hapa, inatoka moja kwa moja kutoka Wikidata.

Ili kubadilisha au kuhariri data inayoonekana kwenye databox:

  1. Bonyeza alama ya penseli Alama kutoka maktaba ya OOjs UI. kando ya maelezo kwenye databox.
  2. Hii itakupeleka mahali ambapo maelezo hayo yamehifadhiwa kwenye Wikidata.
  3. Bonyeza alama ya penseli Alama kutoka maktaba ya OOjs UI. tena, upande wa kisanduku cha Maelezo (Statement). Hii itafungua hali ya kuhariri kule Wikidata.
    • Ingiza thamani mpya kwenye sehemu ya kuandikia. Ongeza sifa za ziada (qualifiers) au marejeo kama inavyostahili.
    • Ikiwa thamani imepitwa na wakati lakini bado ni sahihi (kama data ya Sensa), bonyeza alama ya + iliyo upande wa kulia wa alama ya penseli, na uingize thamani mpya zaidi.
  4. Bonyeza kitufe cha alama ya vema ili kuchapisha maelezo. Databox itajisasisha mara moja na habari mpya itaonekana.


Mifano ya Databox

[hariri chanzo]
{{Databox|item=Q42}}
Kigezo:Databox
kigezo cha Wikimedia

Mifano hapa chini inaonyesha jinsi kigezo cha databox kinavyoweza kuonekana katika mwonekano wa kuhariri msimbo (edit source).

  • {{Databox}}
Chaguo la kawaida. Itachukua data kutoka kwenye kipengele cha Wikidata kilichounganishwa na ukurasa.
  • {{Databox|item=Q123}}
Inalazimisha databox kuchukua data kutoka kwa kipengele maalum cha Wikidata. Hii inaweza kuwa kipengele tofauti na kile kilichounganishwa na ukurasa, lakini haiwezi kuwa vyote viwili. Data ya databox inaweza tu kuchukuliwa kutoka kwa kipengele kimoja.
  • {{Databox|useImage=jinalapicha.jpg}}
Chagua picha nyingine kwa mikono (P18) ili ionekane kwenye databox.
  • {{Databox|excludeProperties=P123}}
Onyesha orodha ya sifa za Wikidata (PID's) zilizotenganishwa kwa mkato ambazo hazitakiwi kuonekana kwenye databox ya sasa.
  • {{Databox|useImage=jinalapicha.jpg|excludeProperties=P123}}
Kuunganisha vigezo hivi kunaruhusu udhibiti zaidi wa maudhui.

Hakuna maelezo.

Vipengele vya kigezo[Hariri data za kigezo]

KipengeleMaelezoAinaHali
useImageuseImage

Jina la faili la picha unayopendelea kutumia kutoka Wikidata Entity

Kishazihiari
excludePropertiesexcludeProperties

Orodha ya Id za Sifa za Wikidata zilizotenganishwa kwa mkato ili kuziondoa kwenye databox

Kishazihiari


Jinsi ya kutumia vigezo vipya

[hariri chanzo]

Maelekezo ya hatua kwa hatua ya kutumia vigezo vya ziada vya Databox.

useImage

[hariri chanzo]
  1. Fungua mwonekano wa kuhariri msimbo wa ukurasa unaotaka kuongeza Databox, au hariri iliyopo tayari.
  2. Ongeza msimbo huu: |useImage=kwenye kigezo cha {{Databox}}.
  3. Nenda kwenye kipengele cha Wikidata cha databox husika, na utafute maelezo ya Picha (P18). Kidokezo: unaweza kuongeza #P18 mwishoni mwa URL ya kipengele cha Wikidata ili kufika hapo haraka.
  4. Ili kutumia picha tofauti (ndani ya Wikipedia) na ile inayotumika sasa, tafuta jina la faili (chini ya picha yenyewe) na likoleze kisha linakili (Ctrl+C).
  5. Rudi kwenye ukurasa ambapo unaitisha {{Databox|useImage=}} na udondoshe (Ctrl+V) jina la faili ulilonakili ndani ya kigezo.
  6. Msimbo wa kigezo sasa unapaswa kuonekana hivi:
    {{Databox|useImage=maandishi_yaliyokolezwa.jpg}}
  7. Hakiki mabadiliko ili kuona picha mpya kwenye Databox, na chapisha ukurasa ili kuhifadhi mabadiliko yako.

excludeProperties

[hariri chanzo]
  1. Ongeza {{Databox}} kwenye ukurasa au tazama iliyopo, na uandike pembeni ID/namba ya Sifa (Property ID) ya mistari na data unayotaka kuificha kutoka kwenye databox ya hapa.
    1. Unaweza kufanya hivyo haraka kwa kupitisha mshale wa panya (mouse) juu ya alama ya kwenye mstari husika wa databox.
    2. Chini ya dirisha la kivinjari chako (browser), URL ya sifa husika itaonekana; tafuta na uandike PID ya URL hiyo.
      Mfano: ikiwa URL inaonekana kama
      www.wikidata.org/wiki/Q123456#P789, andika P789.
    3. Fanya vivyo hivyo kwa mistari/sifa zote zinazopaswa kufichwa.
  2. Ongeza msimbo huu:
    |excludeProperties=kwenye kigezo cha {{Databox}}.
  3. Ongeza ID/namba za Sifa kwenye msimbo wa kigezo cha databox, zikitenganishwa kwa mkato , k.m.
    {{Databox|excludeProperties=P789,P123,P456}}
  4. Hakiki mabadiliko ili kuhakikisha mistari imefichwa kwenye databox, na chapisha ukurasa ili kuhifadhi mabadiliko yako.

Tafadhali kumbuka: Kigezo hiki huficha tu data ya sifa, haiondoi au kuifuta na haitaathiri Databox nyingine zozote kwenye Wikipedia hii au Wikipedia nyingine.