Kievenki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kievenki ni lugha ya Kitungusi nchini Uchina, Urusi na Mongolia inayozungumzwa na Waevenki. Mwaka wa 2007 idadi ya wasemaji wa Kievenki nchini Uchina imehesabiwa kuwa watu 11,000. Pia kuna wasemaji 4800 nchini Urusi (2010) na 1000 nchini Mongolia (1992). Kufuatana na uainishaji wa lugha, Kievenki iko katika kundi la Kitungusi ya Kaskazini. Nchini uchina Kievenki huandikwa na alfabeti ya Kimongoli. Nchini Urusi, Kievenki imeandikwa na alfabeti ya Kikirili tangu 1937.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kievenki kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.