Kidahalo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kidahalo ni lugha ya Kiafrika-Kiasia nchini Kenya inayozungumzwa na Wadahalo. Mwaka wa 1992 idadi ya wasemaji wa Kidahalo imehesabiwa kuwa watu 400 tu. Hata hivyo, kuna Wadahalo 3000 lakini wengi hutumia Kiswahili badala ya lugha yao ya Kidahalo, maana yake Kidahalo kiko hatarini mwa kutoweka. Kufuatana na uainishaji wa lugha kwa ndani zaidi, Kidahalo iko katika kundi la Kikushi.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kidahalo kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.