Kibali (tamthiliya)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kibali ni tamthilia ya kwanza na David Kyeu. Imechapishwa mwaka wa 2010. Katika tamthilia hii, Kisasa, mwanamke aliyesoma anampeleka mumewe mahakamani akitaka talaka kwa sababu mumewe amembaka. Mumuwe haamini kwamba katika ndoa ubakaji unaweza kutokea na majaji wanaonekana kuegemea upande wake. Kisasa baadaye anafaulu katika mahakama tofauti. Anajiunga na kundi la wanawake mahanithi (lesbians), anakuwa malaya baadaye anakuja kuuawa na mwanawe Boi ambaye anadai yeye ni mwanamume na upuzi wa wanawake hataki.