Nenda kwa yaliyomo

Kiawentiio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kiawenti:io Tarbell [1] (maarufu kwa jina Kiawentiio; alizaliwa 28 Aprili 2006)[2][3] ni mwigizaji kutoka Waindio Wamohawk, mwanamuziki na mtunzi wa nyimbo.

Alianza kuigiza katika msimu wa tatu wa tamthilia ya CBC series iitwayo Anne with an E (2019) na filamu yake ya kwanza ikiwa Beans (2020). Aliigiza kama Maya Thomas katika sitcom Rutherford Falls (2021). Alichaguliwa kuigiza kama Katara katika tamthilia ya Avatar: The Last Airbender (2024).

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Kiawentiio alizaliwa katika familia ya Mohawk huko Akwesasne, ambayo ni hifadhi ya kwanza ya taifa iliopakana na nchi zote Canada na Marekani na kuzungukwa na mto St Lawrence[4][5]. Kwa upande wa Marekani inajulikana kama hifadhi ya St Regis Mohawk.

Jina lake la kwanza lina maanisha "Asubuhi njema" huko Kanienʼkéha[6]. Wazazi wake ni Barbara na Corey Tarbell. Amekulia katika nyumba ya Kawehno:ke ( pia inajulikana kama Cornwall Island) na kusoma shule ya Uhuru ya Akwesasne na Shule ya Ufundi ya Cornwall Collegiate. Ana uraia wa nchi mbili Canada na Marekani.

Tarbell alikuwa mmoja wa waigizaji 200 wenye asili ya Kanada kwa ajili ya kuigiza kama Ka'kwet, ambae ameonyeshwa katika msimu wa tatu wa tamthilia ya Anne with an E. Alilazimika kujifunza lugha ya Mi'kmaq na kuelewa utamaduni na historia ya hilo kabila. Pia aligiza katika filamu ya Beans 2020 kama msichana wa Mohawk mwenye umri wa miaka 12 aliekua anaishi Kahnawake mnamo 1990, kipindi cha Mgogoro wa Oka.

Ameonekana kama muhusika wa mara kwa mara akiwa kama Maya Thomas kwenye tamthilia ya Peacock sitcom Rutherford Falls (2021). Pia alichagulia kuvaa uhusika wa Katara katika tamthilia ya Avatar: The Last Airbender series.

  1. https://www.cbc.ca/kidsnews/post/rising-star-meet-kiawentiio-tarbell-new-star-on-anne-with-an-e
  2. "Instagram". www.instagram.com. Iliwekwa mnamo 2024-04-03.
  3. "Kiawentiio - Actress". TV Insider (kwa American English). 2024-02-22. Iliwekwa mnamo 2024-04-03.
  4. https://www.tribute.ca/people/biography/kiawentiio/59990/
  5. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2024-02-03. Iliwekwa mnamo 2024-04-03.
  6. https://perchmagazine.com/acting-up/
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiawentiio kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.