Nenda kwa yaliyomo

Kesi za Nuremberg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kesi za Nuremburg. Wahalifu kizimbani. Mhalifu mkuu aliyelengwa hapa alikuwa ni Hermann Göring (upande wa kushoto katika mstari wa viti wa kwanza), anayedhaniwa kuwa afisa muhimu zaidi aliye hai wa Jamhuri ya tatu baada ya kifo cha Adolf Hitler.

Kesi za Nuremburg zilikuwa mfululizo wa kesi za kijeshi ambazo zilifahamika sana kwa kuwahukumu wanachama wakuu wa kuongoza Ujerumani ya Kinaksi kisiasa, kijeshi, na kiuchumi baada ya Ujerumani kushindwa katikia Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.

Kesi hizo zilifanywa katika mji wa Nuremburg, Ujerumani, kuanzia mwaka wa 1945 hadi mwaka wa 1946, katika Kasri la Haki. Kesi ya kwanza kati ya hizi na inayofahamika sana ilikuwa ni Kesi ya Wahalifu Wakuu wa Vita mbele ya mahakama ya kimataifa ya kijeshi ambapo viongozi 22 Muhimu waliokamatwa katika Ujerumani ya kinaksi walihukumiwa.

Kesi za Nuremburg zilifanywa kati ya tarehe 21 Novemba, mwaka wa 1945 na tarehe 1 Oktoba mwaka wa 1946, seti ya pili ya kesi iliyokuwa ya wahalifu wenye mashtaka madogo ilifanywa chini ya Sheria ya Baraza la Udhibiti, nambari 10, mbele ya Mahakama ya Kijeshi ya Nuremburg nchini Marekani; miongoni mwa kesi hizo ni Kesi za madaktari na Kesi za Mahakimu.

Makala hii kuhusu mambo ya kihistoria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kesi za Nuremberg kama enzi zake au matokeo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.