Nenda kwa yaliyomo

Kerry Washington

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kerry Marisa Washington
Washington at the Django Unchained premiere in 2012
Washington at the Django Unchained premiere in 2012
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Kerry Marisa Washington
Amezaliwa Januari 31 1977 (1977-01-31) (umri 47)
Kazi yake Actress

Kerry Marisa Washington (aliyezaliwa 31 Januari 1977) ni mwigizaji wa Marekani.

Tangu mwaka 2012, Washington amepata umaarufu kutokana na kuwa nyota katika mchezo wa ABC uitwao scandal, tamthilia ya Shonda Rhimes ambayo huchezwa na Olivia Pope, mtaalamu wa utatuzi wa migogoro kwa wanasiasa na wanasheria wa nguvu huko Washington DC. Kwa nafasi alizocheza, amechaguliwa mara mbili kwenye tuzo ziitwazo Primitime Emmy awards kama muigizaji bora wa michezo ya tamthilia, Tuzo za sreen actor Guild kama Mwanamke bora wa mchezo wa tamthilia, na Tuzo za Golden Globe kama muigizaji bora katika Televisheni . Washington pia anajulikana kwa nafasi yake alocheza kama Della Bea Robinson, katika filamu iitwayo Ray (2004), kama Kay katika The Last King of Scotland (2006), kama Alicia Masters katika filamu ya Live Fantastic four filamu ya 2005 na 2007, na kama Broomhilda von Schaft katika Django Unchained ya Quentin Tarantino (2012).

Pia amejitokeza katika filamu za kujitegemea our song (2000), The Dead Girl (2006), Mother and child (2009) na Night Catches Us (2010). Mnamo mwaka wa 2016, alichaguliwa kuigiza kama Anita Hill katika filamu ya HBO ya televisheni na alipewa Tuzo za primetime Emmy award muigizaji bora wa tamthilia na Mwandishi bora wa Kisasa.

Mnamo Aprili 2014, gazeti la Time lilimtaja Washington kwenye orodha ya "Time 100" ya kila mwaka.

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kerry Washington kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.