Kazunori Yamauchi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Kazunori Yamauchi

Kazunori Yamauchi(Kijapani: 山内 一典, amezaliwa 5 Agosti 1967) ni muundaji wa michezo ya video kutoka nchi ya Japan ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Polyphony Digital na muumba na mtayarishaji wa mchezo maarufu unaoitwa Gran Turismo. Alipata cheo cha rais katika PolyPhony Digital baada ya kujenga mchezo wake wa kwanza unaoitwa Motor Toon Grand Prix mchezo ambao ulikuwa asili kabisa na wa kipekee. Tangu hapo, Yamauchi ametimiza ndoto yake ya kuunda mchezo bora wa gari kupitia kwa mafanikio yaGran Turismo .

Kwa msaada wake katika kukuza gari aina ya Volkswagen (VW) katika mchezo aliounda, alituzwa gari aina ya VW Golf R32.

Hivi karibuni alisaidia kwa kubuni teknolojia mpya wa Nissan GT-R ambayo inaonekana katika toleo jipya ya mchezo, Gran Turismo 5 Dibaji.Alituzwa gari aina ya Nissan GT-R kwa mchango wake.

Katika video Gran Turismo 5: Prologue Yamauchi ametaja kwamba gari anayoipenda zaidi ni GT Ford na anamiliki magari mawili ya aina hii katika maisha halisi.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]