Kampuni ya G.R. Kinney

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kampuni ya GR Kinney
Jina la kampuni Kampuni ya GR Kinney
Ilianzishwa 1984
Mwanzilishi George Romanta Kinney
Huduma zinazowasilishwa Utengenezaji na Uuzaji
Bidhaa zinazosambazwa na kampuni hii Viatu
Nchi Marekani
G.R.Kinney

Kampuni ya GR Kinney ilikuwa kampuni ya uzalishaji na uuzaji wa viatu kutoka mwaka wa 1984 hadi mwezi wa 16 Septemba 1998. Alama yake ya KNN katika orodha ya kampuni katika Soko la Hisa la New York ilianza kutumika Machi 1923.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Wazo la kutengeneza viatu lilianzishwa na George Romanta Kinney ambaye baba yake aliendesha duka la kuuza vitu vyovyote kwa jumla katika eneo la Candor, New York. Baba yake akapatwa na mzigo mkubwa wa madeni na George aliapa kulipa madeni hayo yote katika siku zake za baadaye. Katika mwaka wa 1894, akiwa umri wa miaka 28, kiwango cha pesa alizokuwa akiweka kando kilitosha kununua duka la Lester huko Waverly,New York. Mafanikio ya Kinney yaliletwa na kuuza viatu kwa bei nafuu kwa raia wafanyikazi wa Marekani.

Biashara hii ulikua na ukawa mnyororo wa maduka 362 katika mwisho wa mwaka wa 1929, huku maduka 44 yakifunguliwa katika mwaka wa mwisho katika mwongo huo. Foot Locker lilianza kama mgawanyiko mdogo wa Shirika la Kinney Shoe katika mwaka wa 1974.

Mnyororo na hapo baadaye[hariri | hariri chanzo]

Huu ulikuwa mnyororo mkubwa kabisa wa maduka ya rejareja chini ya usimamizi wa kifamilia nchini Marekani .Tangu mwanzo wa mwaka wa 1936,ulikuwa na maduka 335 katika taifa zima. Ingawa kampuni hii ilipata mauzo mengi hapo mwisho wa mwaka wa 1936 kuliko ilivyouza katika mwaka wa 1929, madola ya mwaka huo(wa 1936) yalikuwa 20%-30% chini ya yaliyopatikana katika mwaka wa 1929.

Tarehe 31 Agosti 1963 ,Kampuni ya GR Kinney iliuzwa kwa F.W. Woolworth. Kabla ya hii, ilikuwa imekuwa shirika dogo la Kampuni ya Viatu ya Brown ndipo Brown ikaliuza kwa bei ya $ milioni 45. Kampuni hii iliitwa Shirika la Viatu la Kinney na likaendelea kuwa shirika dogo katika kampuni ya Woolworth. Bodi yake ya wakurugenzi kumi na mmoja na jopo la maafisa wa kampuni liliendelea kufanya kazi katika Shirika la Kinney.

Foot Locker[hariri | hariri chanzo]

Kampuni iliendelea kuendeshwa katika miaka ya 1960 na 1970 pamoja na migawanyiko yake iliyoitwa Stylco (1967), Susie Casuals (1968), na Foot Locker (1974). Tarehe 16 Septemba 1998, Kundi la Venator lilitangaza kuwa maduka 467 ya viatu na maduka 103 ya Footquarters yangefungwa. Sehemu ya Foot Locker,iliyoanzishwa katika mwaka wa 1974, inaendelea hadi sasa huku Venator ikibadilisha jina lake kuwa Foot Locker katika mwaka wa 2001.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ G.R. Kinney Co. Sales, Wall Street Journal, 9 Aprili 1930,
  2. ^ a b Brown Shoe Co, Wall Street Journal, 3 Desemba 1964,
  3. ^ Topics In Wall Street, New York Times, 30 Machi 1923
  4. ^ a b Kinney Shoe Corporation webpage, internet article.
  5. ^ G.R. Kinney Sales Up, Wall Street Journal, 9 Januari 1930
  6. ^ Kinney Shoe Corporation, makala kwenye mtandao.
  7. ^ G.R. Kinney Shows Net of $22,748 For Last Year, Wall Street Journal, 30 Januari 1936
  8. Kinney Co. Calls Meeting to Eliminate Operating Deficit, Wall Street Journal, 4 Desemba 1936
  9. ^ Investing In Yourself, Wall Street Journal, 30 Juni 1965

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]