Eleveta

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kambarau)

Eleveta (kutoka Kiing. elevator), pia: lifti, kipandishi, kambarau ni chombo cha kupandisha na kushusha watu au mizigo.

Mara nyingi eleveta hutumiwa katika majengo ya ghorofa. Zinatokea pia nje ya majengo kwa mfano katika migodi ambako zinaweza kufika mamia ya ya mamita chini ya ardhi.

Kwa kawaida eleveta ni chumba chenye mlango kinachovutwa kwa kamba au kupandishwa kwa namna ya jeki kati ya ghorofa inapofika. Watu huingia ndani wanapoweza kuchagua ni ghorofa ipi wanapotaka kufika kwa kubofya kitufe ukutani. Milango inafungwa na chumba cha eleveta hupanda au kushuka jinsi inavyotakiwa.

Siku hizi eleveta huendeshwa kwa msaada wa injini ya umeme unaovuta kamba au kuendesha pampu ya jeki. Katika historia kuna mifano ya eleveta zilizoendeshwa kwa nguvu ya kibinadamu au kinyama. Mfano wa kwanza unaojulikana ni eleveta iliyotengenezwa na mtaalamu wa Ugiriki wa Kale o reported Archimedes (mnamo 287 KK – 212 KK) mjini Sirakusa.

Eleveta ndefu duniani ziko ndani ya migodi zinazofikia kimo cha mita maelfu. Eleveta ndefu katika jengo ni ile ndani ya ghorofa la Burj Khalifa la mjini Dubai inayopanda mita 504.