Nenda kwa yaliyomo

Burj Khalifa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Burj Khalifa (kizamani kujulikana kama Burj Dubai) ni jengo kubwa la maghorofa lililojengwa nchini Dubai, Falme za Kiarabu mwaka 2009. Tangu mwaka 2009 ni jengo lenye kimo kikubwa duniani.

Burj Khalifa ina ghorofa 163 na eneo la vyumba vyote ni m2 309,473. Ghorofa ya juu inaishia kwa mita 585.4 na antenna juu yake inafikia mita 829.8. Gharama zilikuwa dola billioni 1.5.

Ghorofa 37 za kwanza ni hoteli. Juu yake kuna makazi 779 katika ghorofa 38-108 na 700 yameshauzwa. Ghorofa za juu zina ofisi na makazi maalumu.

Kutokana na ukubwa na urefu wake, Burji Khalifa husafishwa kwa wiki nane. Kihistoria, Burj Khalifa ilijengwa kwa ajili ya kuliingizia taifa kipato baada ya rais wa Falme za Kiarabu wa wakati ule kuona hakuna kivutio cha watalii nchini humo. Akaamua lijengwe jengo lefu kuliko yote yote ulimwenguni na wakalipa jina la Burj Khalifa.

Picha za ujenzi

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Burj Khalifa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons