Jennifer White-Johnson
Mandhari
Jennifer White-Johnson ni msanii na mwanaharakati anayeishi Baltimore, Maryland, Marekani. Akiwa msanii mlemavu mwenye asili ya Afro-Latina aliye na ADHD na ugonjwa wa Graves, anatumia muundo wa picha na upigaji picha kujadili muunganiko wa haki za walemavu na kupinga ubaguzi wa rangi, na kutoa mwonekano kwa sauti zisizopewa nafasi. Baada ya kumaliza shahada ya uzamili, alifundisha kama profesa wa Usanifu wa Mawasiliano ya Picha katika Chuo Kikuu cha Bowie State. Baadhi ya kazi zake maarufu ni pamoja na alama ya Black Disabled Lives Matter na jarida la utetezi linaloitwa Knox Roxs kuhusu furaha ya watu weusi wenye usonji.[1]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Huertas, Jenny Chang-Rodriguez, Katty. "20 Latino Artists to Watch". www.today.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-09-20.
{{cite web}}
: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Jennifer White-Johnson kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |