Nenda kwa yaliyomo

Indakateroli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Indakateroli (Indacaterol), inayouzwa kwa jina la chapa Onbrez miongoni mwa mengine, ni dawa inayotumika kutibu Ugonjwa sugu wa njia za pumzi zilizofungana (COPD).[1] Dawa hii inatumiwa na kuvutia hewa ya poda kavu mara moja kwa siku.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na maambukizi ya njia ya juu ya upumuaji, maumivu ya kifua na kikohozi.[2] Kwa wale walio na pumu, inaweza kuongeza hatari ya kifo.[1] Ni agonisti ya muda mrefu ya beta-adrenoceptor (LABA).[1]

Indakateroli iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu huko Uropa mnamo mwaka wa 2009, na huko Amerika mnamo mwaka wa 2011.[2][1] Nchini Uingereza, inagharimu Huduma za Afya za Kitaifa (NHS) takriban £32 kwa mwezi kufikia mwaka wa 2021.[3] Nchini Marekani, kiasi hiki kinagharimu takriban dola 260 za Kimarekani.[4]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 "Indacaterol Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 22 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Onbrez Breezhaler". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 28 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. BNF 81: March-September 2021. BMJ Group and the Pharmaceutical Press. 2021. uk. 267. ISBN 978-0857114105.
  4. "Indacaterol Prices, Coupons & Savings Tips - GoodRx". GoodRx. Iliwekwa mnamo 26 Novemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Indakateroli kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.