Ider

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ider ni mto uliopo Mongolia; unapita kati ya Khövsgöl na Zavkhan aimags kaskazini magharibi mwa Mongolia. Pamoja na mto Delgermörön ni vyanzo vya mto Selenge. Una urefu wa kilomita 452 (281 mi), na una beseni la kilomita za mraba 24,600 (9,500 sq mi). Chanzo kiko katika safu za Khangai, ukutana na Delgermörön uko Tömörbulag. Mto huo uganda siku 170-180 kwa mwaka. Kuna daraja la mbao, ambalo lilijengwa mnamo 1940, karibu na Jargalant ni daraja la zege lipo huko Galt.

Daraja la mbao lililopo huko Jargalant.