Nenda kwa yaliyomo

ISAKOS

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Shirika la Kimataifa la Athroskopia, Upasuaji wa Goti na Taaluma ya Tiba ya Mifupa katika Michezo (ISAKOS) ni shirika la taaluma ya tiba lililo na takriban wanachama 4000. Uanachama wake unajumuisha madaktari wapasuaji wa tiba ya mifupa pamoja na wanasayansi wa michezo, madaktari wa michezo na wataalamu wa viungo katika michezo. Wanachama wanatoka katika nchi 92 tofauti tofauti na kila mmoja ni sharti awe mwanachama wa mashirika ya taaluma ya tiba ya mifupa katika michezo ya nchi zao au mashirika ya kimaeneo ulimwenguni ya taaluma ya tiba ya mifupa katika michezo kama vile Shirika la Taaluma ya tiba ya mifupa la Marekani Kaskazini (AANA) , Shirika la Marekani la Taaluma ya Tiba ya mifupa (AOSSM Ilihifadhiwa 23 Julai 2020 kwenye Wayback Machine. ()), Shirika la Asia-Pasifiki la Athroskopia ya goti,na Taaluma ya Tiba ya Spoti (APKASS), Shirika la Ulaya la  Elimu Kiwewe Michezoni, Upasuaji wa goti,na Athroskopia na Shirika la Sociedad Latinoamerikana la Athroskopia na kimahususi Rodilla y Deporte (SLARD)

Madhumuni ya ISAKOS ni kuwa shirika jumuishi la mashirika haya ya kimaeneo na kuwezesha ubadilishanaji wa maarifa baina yao na la muhimu zaidi, kukuza elimu katika nyanja za upasuaji wa goti na taaluma ya tiba ya mifupa kwa maeneo ya dunia ambako fursa ya namna hii ya elimu ni adimu.ISAKOS hufanikisha malengo haya kwa kuwahusisha wanachama katika mikutano ya kielimu, udhamini wa ziara za madaktari wapasuaji kutoka nchi masikini kutembelea vituo vya ubora pamoja na tuzo kadhaa, ruzuku na idhinisho ya mikutano ya kimaeneo.

Athroskopia (pia huitwa upasuaji wa kiathroskopia) ni upasuaji usio wa kina kwenye kiungo  ambapo matibabu yanatekelezwa kwa matumizi ya kifaa kinachoitwa athroskopi kinachoingizwa kupitia chale ndogo.

Tiba ya spoti, inayojulikana pia kama Tiba ya spoti na mazoezi (SEM), ni kitengo cha tiba kinachohusika na kinga na matibabu yanayohusiana na spoti na mazoezi ya viungo.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

ISAKOS ilianzishwa mnamo 1995 kule Hong Kong katika kongamano la pamoja la Shirika la Kimataifa la Athroskopia (IAA) na Shirika la Kimataifa la goti (ISK). Mashirika haya mawili awali yalifanya mikutano yao moja baada ya jingine lakini ilipobainika kuwa wengi wa washiriki walijipata wanahudhuria mikutano yote miwili ikawa ni suala la mantiki  kuiunganisha. ISAKOS ndio muungano wa mashirika haya ya Kimataifa (ISK na IAA). ISAKOS huandaa Kongamano la kimataifa kila mwaka wa pili. Tangu kuanzishwa kwake makongamano haya yamekwisha kufanywa kote Ulimwenguni. Rais wa kwanza wa ISAKOS alikuwa ni  Dkt. Peter, J. Fowler wa Canada aliyehudumu kutoka mwaka wa 1995 hadi 1997.

Katika kipindi cha 2015 -17 shirika hili  lilikuwa chini ya wenyekiti wa Mfaransa, Dkt Phillipe Neyret, aliyefuatwa na Mmarekani, Dkt Marc Safran kutoka mwaka 2017-19. [1] Kwa sasa shirika hili liko chini ya wenyekiti wa Dkt Willem von de Merwe wa Afrika Kusini ambaye ataongoza hadi 2021.[2]

Uanachama

[hariri | hariri chanzo]

ISAKOS ni shirika la kimataifa la watu binafsi ambao kweli wanapendelea Taaluma ya Tiba ya Mifupa Michezoni na nyanja za sayansi na taaluma ya tiba zinazohusiana nayo. Hizi ni kama upasuaji wa goti,upasuaji wa kiathrokospia wa viungo vyote, na taaluma ya tiba ya mifupa katika spoti. Ni kawaida kwa wale wanaowania uanachama kuwa pia wanachama wa mashirika makubwa ya kimaeneo. Haya ni Shirika la Kiathroskopia la Marekani Kaskazini (AANA), Shirika la Marekani la Taaluma ya tiba ya mifupa (AOSSM) . Shirika la Asia-Pasifiki la Athroskopia ya goti,na Taaluma ya Tiba ya Spoti APKASS. Shirika la Ulaya la Taaluma ya Matibabu ya Vidonda na Majeraha Michezoni, Upasuaji wa Goti na Athroskopia (ESSKA) na Shirika la Sociedad Latinoamerikana la Athroscopia na  Rodilla y Deporte (SLARD). Wanachama wa ISAKOS pia ni wanachama  wa mashirika yao ya kimaeneo au  mashirika ya Kitaifa ya taaluma ya tiba ya mifupa katika michezo (au mashirika linganifu). Naam,wanachama wa mashirika haya wanaweza kutunukiwa hadhi ya uanachama shirikishi wa ISAKOS pindi wanapotuma maombi yao.

Kuna makundi mawili ya uanachama:

Wanachama shirikishi

Wale walio na upendeleo au uwezo katika nyanja za tiba au sayansi wakiwa pia na mapendeleo katika athroskopia, upasuaji wa goti na taaluma ya tiba ya mifupa katika michezo wanastahiki.Wanachama kama hawa  hawana haki ya kupiga kura na hawastahiki kupewa vyeo vya ofisi.

Wanachama tendi

Watu binafsi waliofuzu kama madaktari wapasuaji wa tiba ya mifupa,madaktari wapasuaji wa misuligofu, madaktari wa baridi yabisi au tiba nyingine linganifu katika nchi zao na wenye hadhi kitiba katika mashirika ya kitaifa au kimaeneo kama ilivyoamuliwa na kamati ya uanachama ya ISAKOS. Wanachama tendi  wana haki ya kupiga kura katika mikutano yote.ya uanachama na wanastahiki kupewa vyeo katika shirika Uanachama tendi hutuzwa huku wakisubiri mapitio ya maombi yao katika mkutano wa kamati ya kuidhinisha Uanachama. Kamati hii ya kuidhinisha uanachama hukutana  katika mkutano wa kila mwaka wa AAOS na katika makongamano ya ISAKOS.

Ili kukuza ubora katika utafiti na kuwatuza wale waliofanya kazi kwa manufaa ya shirika ISAKOS inatoa tuzo kadhaa. Tuzo huwa katika makongamano yanayofanywa kila mwaka wa pili. Tuzo hizi huwasilishwa katika kongamano na hutaarifiwa katika kijarida cha shirika na pia katika wavuti wa ISAKOS.

Idadi kubwa ya tuzo hizi hutoa shime kwa wanachama mashuhuri wa sasa na zamaniwa ISAKOS na pia viongozi wakongwe watajika wa taaluma ya upasuaji wa michezo  wakati nyingine hutoa misaada ya kifedha kwa utafiti, uanazuoni na mahudhurio katika mikutano iliyodhaminiwa na ISAKOS.

Kwa kufungamana na wito wa kimsingi wa ISAKOS msaada hutolewa kwa mapendeleo, kama msaada kwa  utafiti na usomi kwa watu binafsi kutoka nchi ambako fursa kama hizi huenda zisipatikane.

Tuzo hizi zinajumuisha;

Tuzo

  • Tuzo ya John J. Joyce- Kwa makala bora zaidi ya athroskopia
  • Tuzo ya Richard B. Caspari- Kwa makala bora zaidi kuhusu mikono
  • Tuzo ya Kisayansi ya Jan I. Gillquist- Kwa utafiti bora zaidi wa kisayansi
  • Tuzo ya Gary G. Poehling-  Kwa makala bora zaidi kuhusu kiwiko, kisugudi na mkono
  • Tuzo ya Mchunguzi Mchanga ya Albert Trillat- Kwa mtafiti mchanga   wa maswala ya  Kikliniki
  • Tuzo ya utafiti katika Taaluma ya Tiba ya mifupa ya Kisigino katika Spoti-  Kwa utafiti bora zaidi kuhusu Taaluma ya Tiba katika Spoti
  • Tuzo ya Paolo Aglietti – Kwa utafiti bora zaidi wa Athroplastia ya Goti
  • Tuzo ya utafiti bora kuhusu Fupaja – Kwa utafiti bora zaidi kuhusu Fupaja

Uanazuoni na Ruzuku

  • Uanazuoni tamba wa Ulimwengu wa ISAKOS
  • Uanazuoni tamba wa Fupaja
  • Ruzuku ya Kimataifa ya Kongamano kwa Mwanazuoni waTaaluma ya Tiba ya Spoti
  • Ruzuku ya Kituo cha Mafunzo
  • Kikao cha utafiti kuhusu maswala ya Kikliniki  kinachogharimiwa na ISAKOS
  • Programu ya Ushauri kuhusu Utafiti na Ruzuku Kwa Wachunguzi wachanga inayoendeshwa na ISAKOS

Maombi ya Tuzo na Ruzuku hizi hufanywa mwaka mmoja kabla ya kongamano ambalo hufanywa kila mwaka wa pili.

Shughuli za Kielimu

[hariri | hariri chanzo]

Lengo la kimsingi la ISAKOS ni kuelimisha katika nyanja za Taaluma ya Tiba ya Mifupa katika Michezo, Athroskopia na upasuaji wa goti. Shirika linafanikisha lengo hili kwa njia nne: kongamano la kila miaka miwili,mikutano ya mabingwa inayolenga kupata mwafaka fulani na inayoishia kwa chapisho, kozi za mafunzo na mbinu za upasuaji zinazopatikana  katika wavuti wa ISAKOS na kujihusisha, baada ya kuidhinishwa,na kozi nyingine zilizo na maudhui sawia kote ulimwenguni. ISAKOS pia huruhusu kupigwa chapa kwa programu za uanazuoni na pia hutoa msaada wa kifedha kwa uanazuoni tamba mahususi wa kielimu

Kongamano la kila mwaka wa pili

Hili ndilo tukio muhimu zaidi katika kalenda ya ISAKOS na shughuli nyingi huzungukia mipango na utaratibu wa Kongamano hili la Kimataifa. Kamati nyingi za ISAKOS hupata fursa ya kutoa mchango katika muundo, fomati na maudhui ya kongamano chini ya uangalizi wa Kamati ya Programu na Mwenyekiti wa Programu. Kongamano lenyewe  ni kikao cha makala huru, na taamuli huhitajika miezi 12 awali ya Kongamano. Kuna ushindani mkubwa katika kukubaliwa kwa makala ili kuwasilishwa jukwaani na kwa jinsi hii ubora wa programu huhakikishwa.

Halikadhalika, Kongamano pia huhusisha kozi za mafunzo kuhusu mada mahususi zinzoongozwa na mabingwa wa Kimataifa pamoja na ikisiri za mada pendwa za masuala leo.. Katika miaka ya hivi karibuni Kongamano limetanuka na kuhusisha maonyesho ya upasuaji na warsha tendaji.

Uwasilishaji wa mabango sasa unafanywa kielekroniki na wajumbe hupokea nakala za kielektroniki za uwasilishaji wa mabango hayo wakati wa usajili. Hivi karibuni zaidi Kongamano limeleta programu-tumizi inayowapatia fursa wajumbe kufanya mapitio ya ikisiri na kupanga watakavyojihusisha katika Kongamano.

Kongamano pia  huhusisha vikao vya mijadala juu ya masuala ya kipindi hicho,maonyesho ya kiufundi  na muda wa kufungamana na wajumbe wenza ambayo ni muhimu katika kujenga uhusiano wa kikazi na kirafiki kimataifa.

Kongamano la ISAKOS la kila baada ya mwaka huchukuliwa kama mojawapo ya mikutano ya mbele zaidi ya kimataifa ya shirika la taaluma ya tiba ya mifupa.Linatoa fursa ya kipekee kwa waliohudhuria kuchanga bia,kujadiliana,na kujifunza maendeleo ya hivi punde zaidi katika athroskopia,upasuaji wa goti na taaluma ya tiba katika spoti. Mkutano huo hufanywa kwa jumla ya siku 5, mnamo miezi ya Mei au Juni. Katika mkutano huu tuzo nyingi za ISAKOS hutolewa kwa wale waliojipambanua zaidi katika utafiti wa kikliniki au kimaabara. Mkutano wa hivi punde zaidi ulifanywa Shanghai, Uchina,na ulihusisha zaidi ya wajumbe 4000 kutoka nchi 84 wakiwasilisha makala 256 na mabango ya  Kielektroniki 753.

ISAKOS pia husaidia na kushirikiana na makongamano mengine  mwaka mzima yakilenga majeraha ya goti.au maswala mengine ya kispoti husika. Halikadhalika shirika linatoa pia idhinisho kwa kozi nyingi za kimafunzo kote ulimwenguni.

Mikutano ya mabingwa inayolenga kufikia mwafaka 

Kamati ya Kikliniki ya ISAKOS imeundwa na wanachama kutoka nchi anuwai walio na mapendeleo mamoja.Hii inaibua mazingira mwafaka kwa majadiliano na pia inawezesha kupatikana kwa masuluhisho ya masuala mengi yanayohusiana na maeneo hayo ya utafiti. Mara kwa mara kamati inaweza kuandaa mkutano kwa nia ya kutafuta suluhu ya suala mahususi au kujadili mada mahususi. Mabingwa kutoka kote ulimwenguni,wawe ni wanaISAKOS au la,hualikwa katika mikutano hii na kwa kawaida mwafaka hufikiwa.

Mikutano hii ya kutafuta mwafaka huishia kuibua chapisho la mada husika. Mwafaka kama huu wa kimataifa kuhusu suala lenye ubishi mkubwa unathaminiwa zaidi kuliko maoni ya bingwa mmoja.  

Idadi fulani ya machapisho yaliyozalishwa na ISAKOS na ambayo ni matokeo ya mikutano ya kutafuta mwafaka hupatikana miongoni mwa wajumbe.Mengi yao yamechapishwa katika majarida heshimika ya taaluma ya tiba ya mifupa.

Mihadhara ya kozi zenye mafunzo na video za mbinu za upasuaji

Kupitia kwa tovuti ya ISAKOS na Kiugo- ulimwengu wanachama wanaweza  kutazama video za mafunzo kuhusu mada za wakati huo.Video za mbinu za upasuaji pia zinapatikana.Baadhi ya hizi video zilirekodiwa katika vikao vilivyopita vya makongamano na nyingine zilitolewa na wapaswaji binafsi kwa manufaa ya wanachama wa ISAKOS.

Mikutano iliyoidhinishwa na ISAKOS

Mashirika ya kimaeneo yana mikutano yao ya ndani yakivutia wanachama wao na wajumbe wengine kutoka ndani au nchi nyingine.Mashirika haya ya ndani yanaweza kutuma maombi kwa ISAKOS ili programu zao ziidhinishwe.Hii huamuliwa na kamati ya kisayansi na kama idhinisho itatolewa hutangazwa na shirika la kimaeneo.Matarajio ni kwamba idhinisho kama hiyo huboresha kiwango cha uaminifu wa usayansi wa mkutano ulioidhinishwa.

  1. "Past Presidents". Iliwekwa mnamo 10 Novemba 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "ISAKOS Board of Directors". www.isakos.com. Iliwekwa mnamo 2019-09-08.
  1. Marais wa awali (https://www.isakos.com/about/Past_Presidents)
  2. Halmashauri ya wakurugenzi wa ISAKOS (https://www.isakos .com/about/BOD)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  • Wavuti wa ISAKOS (http://www.isakos.com/)
  • Jarida la kwenye mavuti la ISAKOS (http://jisakos.bmj.com/)