Nenda kwa yaliyomo

Hulda Swai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hulda Shaidi Swai

Hulda Shaidi Swai
Nchi Tanzania
Kazi yake Mtafiti na Profesa wa sayansi

Hulda Shaidi Swai, alizaliwa mwaka 1954, ni mtafiti na Profesa wa sayansi ya maisha na nyenzo za kibiolojia nchini Tanzania. Yeye ni mwanzilishi katika utafiti wa nanomedicine katika maendeleo ya dawa dhidi ya magonjwa ya kuambukiza barani Afrika. Kazi yake inazingatia hasa matumizi ya nanoteknolojia katika dawa za kupambana na malaria.[1]

Maisha ya awali na elimu

[hariri | hariri chanzo]

Swai alizaliwa mwaka 1954 katika kijiji cha Vudee wilayani Same, mkoa wa Kilimanjaro. Alisoma shule za sekondari katika miaka ya 1970, na mwaka 1980 alihitimu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akiwa na shahada katika kemia na takwimu.[2]

Mnamo mwaka 1985, Swai alitunukiwa shahada ya Master of Science katika uhandisi wa kemikali kutoka Chuo Kikuu cha Malkia Mary cha London.[3] Baadaye alipata shahada ya Udaktari (PhD) katika nyenzo za kibiolojia kutoka chuo hicho hicho mwaka 2000.[2]

  1. ↑ Dr. Y (26 Februari 2021). "Professor Hulda Swai of Tanzania Wins Distinguished Science Award: 'Women are as good as men'". AfroLegends.com. Iliwekwa mnamo 27 Machi 2023.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 1 2 "Why scholar left high-paying job abroad to come back home". The Citizen. 23 Desemba 2018. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2023.
  3. ↑ "Dr Hulda Swai". Strathmore University. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-03-27. Iliwekwa mnamo 26 Machi 2023.
Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Hulda Swai kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.