Holly Aprile

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Holly Aprile (alizaliwa Desemba 23, 1969) ni Mmarekani aliyekuwa mchezaji bora wa mpira laini na kwa sasa ni kocha mkuu wa timu ya mpira wa laini ya Louisville.[1] Alicheza mpira wa laini chuoni akiwa katika nafasi ya utility (anayeweza kucheza nafasi mbalimbali) kwa timu ya UMass Minutewomen kutoka mwaka 1989 hadi 1992 katika Atlantic 10 Conference, ambapo alitunukiwa tuzo ya Chipukizi Bora wa Mwaka, Mchezaji Bora wa Mwaka na Mpiga Mpira Bora wa Mwaka katika kipindi chake cha kucheza, pamoja na kutambuliwa kama mchezaji aliyechaguliwa mara nne kwenye kikosi bora cha timu ya konferensi .[2][3]Alikuwa pia kiongozi wa timu hadi kufika kwenye mashindano ya College World Series ya Wanawake ya mwaka 1992, ambapo walifika katika hatua ya nusu fainali.[4] Aprile pia ameteuliwa kuingia kwenye UMass Hall of Fame (ukumbi wa kumbukumbu wa Chuo Kikuu cha UMass). [5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Christine Vogt. "1992-di-all-american-teams--4653 | awards-history | awards". NFCA (kwa en-gb). Iliwekwa mnamo 2023-07-30. 
  2. "2020 softball record book". University of Massachusetts Athletics (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-07-30. 
  3. "(PDF) - Atlantic 10". atlantic10.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-07-30. 
  4. "The Automated ScoreBook - Massachusetts". fs.ncaa.org. Iliwekwa mnamo 2023-07-30. 
  5. "UMass Inducts 2005 Hall Of Fame Class". University of Massachusetts Athletics (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-07-30.