Nenda kwa yaliyomo

Harold Shipman

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Harold Shipman (14 Januari 194613 Januari 2004) alikuwa daktari na mwuuaji mfululizo wa Kiingereza. Anafikiriwa kuwa ameua takriban watu 250 ambao wote ni wagonjwa wake.

Matukio yake

Alipelekwa mahakamani na akakutanika kuwa na makosa ya kuua watu wapatao 15, na baada ya uchunguzi kufanyika akakutanika tena kusababusha vifo vya watu wapatao 235. Alikuwa akipendelea sana kuua watu kwa kutumia nusu kaputi. Wagonjwa aliowaua wengi walikuwa vibibi vizee.

Kifo chake

Wakati alivyokuwa jela, alijiua. Wengi walifurahia baada ya kusikia hayo na hata kuthubutu kusema kwamba, huo ndiyo mfano wa kuigwa kwa wauaji wa mfululizo wengine. Tukio hilo halikuwafurahisha ndugu wa watu waliouliwa ndugu za wao na kufikiria kwamba serikali inawadanganya juu ya tukio hilo.

Shipman alijinyonga na shuka wakati wa usiku wa kuamkia siku yake ya kuzaliwa, yaani ilikuwa saa sita na dakika ishirini ya kuamkia tarehe 14 Januari ya mwaka wa 2004. Alikutanika na mhudumu wa gerezani na kuanza kutoka taarifa kwamba, Shipman amejinyonga katika nondo za dirisha kwa kutumia shuka la kulalia.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Harold Shipman kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.