Grand Theft Auto Advance

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Grand Theft Auto Advance ni mchezo wa video ulioundwa na Digital Eclipse na kuchapishwa na Rockstar Games kwa ajili ya Game Boy Advance, uliyotolewa mnamo 26 Oktoba 2004.

Maelezo ya mchezo[hariri | hariri chanzo]

Mchezo una hadithi nyingine. Mhusika mkuu sio tena Claude bali ni mhusika mpya anayeitwa Mike.

Baadhi ya wahusika kutoka kwenye mchezo wa Grand Theft Auto III wanaonekana kwenye mchezo huu, pamoja na mmiliki wa duka la mabomu, 8-Ball na bosi anayeongoza uhalifu unaofanywa na kundi la yakuza, Asuka.

Ingawa hakuna mhusika wa Mafia kutoka Grand Theft Auto III aliyejitokeza, wahusika wapya kama Vinnie (Rafiki wa Mike), Cisco na Yuka (mpwa wa Asuka) wameongezwa kwenye mchezo huu.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Sports icon.png Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Grand Theft Auto Advance kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.