Giovanni Tedesco
Giovanni Tedesco | ||
Maelezo binafsi | ||
---|---|---|
Jina kamili | Giovanni Tedesco | |
Tarehe ya kuzaliwa | 13 Mei 1972 | |
Mahala pa kuzaliwa | Palermo, Uitalia | |
Urefu | 1.70m | |
Nafasi anayochezea | Mchezaji wa kati | |
Maelezo ya klabu | ||
Klabu ya sasa | Palermo klabu ya jiji lake nyumbani | |
Namba | 4 | |
Klabu za ukubwani | ||
Miaka | Klabu | |
1990-1993 1993-1995 1995-1997 1997-1998 1998-2004 2004-2006 2006- |
Reggina ACF Fiorentina Foggio Salernitana Perugia Genoa Palermo | |
* Magoli alioshinda |
Giovanni Tedesco (alizaliwa 13 Mei 1972 katika mji wa Palermo) ni mwanakandanda wa Italia. Alikuwa mchezaji wa kati.
Wasifu wa Klabu
[hariri | hariri chanzo]Licha ya kuwa raia wa Palermo, Tedesco ,hapo awali alikatazwa kucheza katika timu ya mji wao,Palermo, kwa sababu mwili wake ulikuwa mdogo na hivyo basi akahamishwa klabu ya Reggina. Akiwa Reggina, alicheza mara kwa mara katika mwaka wa 1990. Baada ya misimu mitatu katika timu ya Reggina (msimu mmoja katika Serie B, na miwili katika Serie C1), Tedesco alihamia klabu ya Fiorentina katika mwaka wa 1993 na akasaidia timu hiyo kushinda Ligi ya Serie B. Katika msimu uliofuata,alicheza kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya Serie A waliposhinda 2-1 katika mechi dhidi ya Cagliari mnamo 4 Septemba 1994.
Baadaye,Tedesco alichezea pia klabu za Foggia,Salernitana na Perugia,alikocheza misimu sita na akapata umaarufu kama mchezaji wa kati na kiongozi wa timu ,hasa akiwa chini ya meneja Serse Cosmi.
Katika mwezi wa Januari 2004, Tedesco aliajiriwa na klabu ya Genoa ya ligi ya Serie B,wakitaka kuimarisha katika timu katika mwisho wa msimu,ambapo timu hiyo(rossoblu) ilikuwa iking'ang'ana kurudi Ligi Kuu ya Serie A. Hata hivyo, Tedesco alianza kucheza vizuri wakati Serse Cormi,kocha wake wa zamani akiwa Perugia, alipokuwa kocha wa Genoa.Serse alichukua nafasi yake Luigi de Canio ambaye hakuweza kufanya klabu hiyo kufanikiwa. Genoa,hatimaye, ilishinda ligi ya Serie B katika mwaka wa 2005. Hata hivyo,klabu ilikataliwa kupandishwa kuenda ligi ya Serie A na badala yake kurudishwa ligi ya Serie C1 kwa kushtakiwa kwa kosa la kufanya udanganyifu uliowasaidia kushinda mechi zao. Baada ya kurudishwa ligi ya Serie C1,Tedesco alichagua kuendelea kucheza katika klabu hiyo kwa nusu ya msimu wa 2005-2006 kabla ya kutia saini mkataba ,ambao hakuweza kukataa, na klabu ya Palermo.
Mnamo 8 Januari 2006, Tedesco alicheza katika mechi yake ya 500, mechi katika uwanja wao wa nyumbani dhidi ya Lazio. Walishinda mechi hiyo 3-1 huku akifunga bao la pili. Mkataba wake na Palermo,uliofaa kuisha Juni 2007, ulirefushwa kwa mwaka mmoja baada ya mechi ya mwisho ya msimu. Iliripotiwa,hapo baadaye, kuwa alikataa mikataba na klabu zingine ili aendelee kucheza katika klabu ya Palermo alipotarajiwa kufunga kazi ya kucheza katikaa klabu hiyo. Tarehe 10 Aprili 2008, yeye alikubaliana masharti ya mkataba wake na Palermo ya kuongeza mwaka mmoja na rosanero.
Katika mwaka wa 2008-09, alihusika kidogo tu, alicheza mechi 17 huku nyingi za mechi hizo zikiwa katika mwisho wa msimu. Mnamo Juni 2009, klabu ilitangaza kurefushwa kwa mkataba na Tedesco,shujaa anayependwa katika mji wao, hadi Juni 2011.
Maisha ya Kibinafsi
[hariri | hariri chanzo]Giovanni Tedesco ana kaka wawili ambao ni wachezaji wa soka:Salvatore (mchezaji wa zamani wa Perugia na Lucchese) na Giacomo, ambaye ni mchezaji wa Reggina.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ^ "Tedesco pens new deal". Football Italia. 2007-05-28. Lugha ya Kiingereza
- ^ "Tedesco:"Mi sono arrivate tante offerte"" Lugha ya Kiitaliano. Stadionews.it. 2007-05-31.
- ^ "Prolungato il contratto di Tedesco" Lugha ya Kiitaliano. US Città di Palermo. 2008-04-10. http://www.ilpalermocalcio.it/it/0708/news_scheda.jsp?id=8799 Archived 11 Julai 2015 at the Wayback Machine.. 2008-04-10.
- ^ "GIOVANNI TEDESCO AL PALERMO PER ALTRI DUE ANNI" Lugha ya Kiitaliano
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Tedesco(katika tovuti ya US Palermo) Archived 30 Aprili 2008 at the Wayback Machine.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Giovanni Tedesco kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |