Gal Gadot

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Gal Gadot katika Mashindano ya 13 ya Kimataifa ya Comic-Con 2018

Gal Gadot Varsano [1][2][3](Alizaliwa Aprili 30, 1985[4][5]) ni mwigizaji na mwanamitindo wa Israeli. Alitawazwa kuwa Miss Israeli 2004 na aliwakilisha Israeli katika mashindano ya Miss Universe 2004. Alihudumia Jeshi la Ulinzi la Israeli kwa miaka miwili akiwa kama mwalimu wa mazoezi ya kupigana, na baadae alianza kusoma katika IDC Herzliya huku akiwa anajitengenezea umaarufu katika uigizaji na uanamitindo.[6][7][8]

Filamu yake ya kwanza ya kimataifa aliyofanya ilikua Fast & Furious (2009) akiigiza kama Gisele Yashar. Gadot alipata umaarufu kimataifa alivyoigiza kama Wonder Woman katika filamu za DC Extended Universe (2016-2023), pamoja na filamu kama Batman v Superman: Dawn of Justice (2016), Wonder Woman, Justice League ( 2017), na Wonder Woman 1984 (2020). Baada ya hapo ameigiza katika filamu za Netflix kama Red Notice (2021) na Death on the Nile (2022).

Gadot aliorodheshwa katika watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani mwaka 2018, na amekua nafasi ya pili kwa waigizaji wanaolipwa zaidi duniani.

Gadot was included on the list of the 100 most influential people in the world by Time in 2018, and has placed twice in annual rankings of the world's highest-paid actresses.

Gadot alijumuishwa kwenye orodha ya watu 100 wenye ushawishi mkubwa duniani kwa wakati mwaka 2018, na ameweka mara mbili katika viwango vya kila mwaka vya waigizaji wanaolipwa zaidi duniani.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://pplus.ynet.co.il/articles/0,7340,L-4886627,00.html
  2. https://www.cosmopolitan.com/entertainment/celebs/a9868643/gal-gadot-wonder-woman-facts/
  3. http://pplus.ynet.co.il/articles/0,7340,L-4886627,00.html
  4. https://www.youtube.com/watch?v=208qNSQTyE4
  5. https://www.upi.com/Top_News/2020/04/30/UPI-Almanac-for-Thursday-April-30-2020/4051588083135/
  6. https://www.gq.com/story/the-gal-gadot-next-door-profile
  7. http://www.ynet.co.il/articles/0,7340,L-3868197,00.html
  8. https://www.wmagazine.com/story/gal-gadot-wonder-woman-beyonce
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Gal Gadot kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.