Nenda kwa yaliyomo

Fatuma (filamu)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Filamu ya fatuma ni tamthilia ya kitanzania ya mwaka 2018 ikiongonzwa na muongozaji wa filamu pia mtayarishaji Jordan Ribe . muongozaji wa hii filamu alishirikiana na wazazi wake kuandaa hii filamu ambao ni John Riber and Louise Riber [1]. kabla ya hii filamu kulikuwa na matangazo ya moja kwa moja yaliokuwa yanarushwa redioni kama maigizo ambayo ni Hadithi za kumekucha,TUNU ambapo filamu ya fatuma imeichukua kisa cha hicho igizo na kufanya kama maudhui ya tamhilia. hii filamu ilikuwa na waigizaji kama Beatrice Taisano, Ayoub Bombwe, Cathryn Credo na wengineyo ila hawa ni kama wahusika wakuu katika tamthilia hii.

Filamu hii inaelezea maisha ya mwanamke wa kijijini na mwanae aliyeolewa na mwanaume ambae alikuwa amampa changamoto mbalimbali. filamu hii iliigizwa mkoani Arusha,Tanzania. Pia filamu hii ilivutiwa na matangazo ya moja kwa moja ya igizo lilokuwa linaarushwa katika redio inayoitwa kumekucha mwaka 2017

FILAMU: Fatuma
Muongozaji wa filamu Jordan Riber
Waandishi Jordan Riber

Andrew Whaley

Waliotayarisha filamu Jordan Riber

John Riber Louise Riber

Wahusika wakuu Ayoub Bombwe

Cathryn Credo Beatrice Taisamo

mtayarishaji wa sinema Talib Rasmussen
Wahariri Jordan Riber

Louise Riber

Mziki Jordan Riber
Wasambazaji wa filamu Media for Development International (MFDI)
Kutolewa 1 Mei 2018 (Tanzania)
Muda Dakika 85
Nchi Tanzania
lugha Swahili

Filamu ya fatuma imepata tuzo mbalimbali za kitaifa katika tamasha la filamu za swahili lilofanyika mwaka 2018 .Tuzo hizo ni kama zifuatazo. Filamu bora yenye picha nzuri, Muongozaji bora wa filamu ambaye ni Jordan Riber, Filamu bora ya sinema na Muigizaji bora wa kike ambaye ni Catherine Credo.

Wahusika

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]

Filamu ya Fatuma katika IMDb

Kava ya filamu

  1. https://www.bing.com/ck/a?!&&p=8190f022e52fa0b3JmltdHM9MTY4NDQ1NDQwMCZpZ3VpZD0wNjJmMzRlYi03NWU0LTYxMDMtMGQzMC0yNjQxNzQ1NjYwYTgmaW5zaWQ9NTIwMw&ptn=3&hsh=3&fclid=062f34eb-75e4-6103-0d30-2641745660a8&psq=catheryn+credo&u=a1aHR0cHM6Ly93aWtpdHJ1c3RlZC5jb20vY2F0aHJ5bi1jcmVkby13aWtpcGVkaWEv&ntb=1