Faith Muthambi
Azwihangwisi Faith Muthambi (alizaliwa 19 Februari 1974) ni mwanasiasa kutoka Afrika Kusini anaewakilisha chama cha African National Congress (ANC) katika mkutano mkuu wa Afrika Kusini. Alikua waziri wa mambo ya ndani kabla ya kuwa waziri wa mawasiliano chini ya raisi Jacob Zuma. Alirudi kwenye mkutano mkuu wa serikali juni 2024 baada ya kuwa katika kiti hicho mnamo mwaka 2009 na 2022.
Maisha na elimu
[hariri | hariri chanzo]Muthambi alizaliwa februari 19 mwaka 1974.[1] Alikua mwanafunzi mwanaharakati wa kwanza katika kongamano kuu Afrika la wanafunzi mnambo mwaka 1989 na 1990 na baada ya hapo kongamano hilo lilizuiliwa kufanyika mwaka 1990. alikua katibu wa tawi la ANC vijana pale Tshimbupfe kaskazini mwa Transvaal(ijulikanayo kama limpopo kwa sasa) kuanzia mwaka 1991 mpaka 1992, na baada ya hapo alijiunga na tawi kuu la ANC Tshimbupfe mwaka 1992.[2]
Kuanzia mwaka 1993 mpaka 1996, alikua mwanafunzi katika chuo kikuu cha Venda, na aliendelea kupanda vyeo ANC ambapo alifanikiwa kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa ANC tawi la Vuwani.[3] Alifanikiwa kuhitumu masomo yake mwaka 1996.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ https://www.gov.za/sites/default/files/gcis_document/201905/42460gen267.pdf
- ↑ https://www.gov.za/sites/default/files/gcis_document/201905/42460gen267.pdf
- ↑ "*** ANC Parliamentary Caucus ****". web.archive.org. 2014-05-27. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-05-27. Iliwekwa mnamo 2024-09-28.
- ↑ "*** ANC Parliamentary Caucus ****". web.archive.org. 2014-05-27. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-05-27. Iliwekwa mnamo 2024-09-28.