Fadumo Dayib
Fadumo Qasim Dayib, ajulikanae kama Deego linalomaanisha "zawadi" kwa Kisomali. ni mwanasiasa kutokea Somalia na ndiye aliekua mwanamke wa kwanza kuogombea uraisi katika uchaguzi wa mwaka 2016.
Maisha na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Dayib alizaliwa mwaka 1972 nchini Kenya.[1][2] Mama yake alisafiri kwenda Kenya baada ya kupoteza watoto kumi na moja kutoka na magonjwa mbalimbali yasiozuilika.[3] Baba yake alikua dereva wa magari ya mizigo na ndie aliewasaidia mama yake na kaka yake kufika Kenya. Walioana wakielekea Kenya na wakaweka makazi yao Thika. Wazazi wake wote wawili hawakua wasomi lakini baba yake alikua ananaongea lugha mbalimbali. Na mama yake aliku mjasiriamali mdogo aliekua akiuza chai bembezoni mwa barabara. Dayib alikua na ndugu wawili waliozaliwa Kenya pia. Wazazi wake waliachana akiwa bado ni mdogo na familia yake iliondolewa Kenya na kurudishwa Mogadishu. Mama yake alifungwa kwa muda baada ya kaka yake kushukiwa kushiriki kuwawezesha vikundi vilivyokua vikimpinga Siad Barre. Mama yake alilazimika kuuza kikla kitu ili wahamie Finland kama wakimbizi ambako ndipo walipoishi tangu mwaka 1990.[4]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Hussein, Leyla (2016-10-12), "Somalia's female presidential candidate: 'If loving my land means I die, so be it'", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2024-09-28
- ↑ Jonathan Lowe (2016-08-11). "Who is Fadumo Dayib, Somalia's first female presidential hopeful?". International Business Times UK (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-09-28.
- ↑ Burke, Jason (2016-09-08), "Somali refugee Fadumo Dayib runs for president 26 years after fleeing civil war", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2024-09-28
- ↑ "First female in Somalia's history to run for president", ABC News (kwa Australian English), 2016-10-12, iliwekwa mnamo 2024-09-28