Eva Mends
Eva Esselba Mends ni mchumi kutoka nchini Ghana. Ndiye mwanamke wa kwanza wa Ghana kuteuliwa kuwa mkurugenzi wa bajeti katika Wizara ya Fedha ya Ghana. Aliteuliwa katika nafasi hiyo mnamo Mei 2017 na serikali.[1][2][3][4][5][6]
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Alisoma katika Chuo Kikuu cha Ghana na kupata shahada katika Sayansi ya Siasa na Uchumi. Aidha, ana shahada ya uzamili ya utawala wa umma (Executive Master's Degree) kutoka katika Chuo cha Taifa cha Usimamizi na Utawala wa Umma cha Ghana. Pia, alihudhuria kozi fupi katika vyuo vya Harvard na Duke.[1][3][4][6]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Mends alianza kazi yake katika Wizara ya fedha kama mtaalamu wa huduma za kitaifa mnamo 1991. Tangu wakati huo, alihudumu katika nafasi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Marekani mnamo 1998, Mkuu wa Maendeleo ya Bajeti mnamo 2006, na Mkuu wa Kikundi cha Marekebisho ya Usimamizi wa Fedha za Umma mnamo 2013. Mnamo Mei 2017, aliteuliwa kuwa mkurugenzi wa bajeti katika Wizara ya Fedha, nafasi aliyoshikilia hadi Januari 2019. Anatambulika kwa kuongoza mabadiliko makubwa, ikiwa ni pamoja na uandaaji wa bajeti unaozingatia jinsia, Bajeti Inayozingatia Programu, na maendeleo ya Sheria mpya ya Usimamizi wa Fedha za Umma. Kwa sasa, yeye ni mkurugenzi mratibu wa Wizara ya Fedha.[2][7][8][9][5][6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 "Eva Mends appointed first female Director of Budget". www.myjoyonline.com. 2017-05-11. Iliwekwa mnamo 2019-11-10.
- ↑ 2.0 2.1 "Late Agyarko's wife removed as Director of Budget at Finance Ministry". www.ghanaweb.com (kwa Kiingereza). 2 Januari 2019. Iliwekwa mnamo 2019-11-10.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 3.0 3.1 "Eva Mends named as first female Director of Budget". Citi 97.3 FM - Relevant Radio. Always (kwa American English). 2017-05-11. Iliwekwa mnamo 2019-11-10.
- ↑ 4.0 4.1 "Eva Mends appointed first female Director of Budget". Graphic Online (kwa Kiingereza (Uingereza)). 2017-05-12. Iliwekwa mnamo 2019-11-10.
- ↑ 5.0 5.1 Ayitey, Charles (2017-05-12). "Gov't has just appointed Ghana's first female director of budgets". Yen.com.gh - Ghana news. (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-11. Iliwekwa mnamo 2019-11-11.
- ↑ 6.0 6.1 6.2 "Eva Mends appointed first female Director of Budget". www.ghanaweb.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-11-11. Iliwekwa mnamo 2019-11-11.
- ↑ "Eva Mends | Ministry of Finance | Ghana". www.mofep.gov.gh. Iliwekwa mnamo 2019-11-10.
- ↑ "Michael Ayesu And Eva Esselba Mends Appointed Finance Ministry Coordinating Directors". Modern Ghana (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-11-10.
- ↑ "Finance Ministry re-organized; gets two new directors". ghananewsagency.org. Iliwekwa mnamo 2019-11-10.