Nenda kwa yaliyomo

Erzgebirge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Erzgebirge

Erzgebirge (jer. tamka erts-ge-bir-ge, milima ya madini, Kicheki Krušné hory) ni safu ya milima iliyopo mpakani wa Ujerumani na Ucheki yenye urefu wa kilomita 150. Upande wa Ujerumani iko katika jimbo la Saksonia, upande wa Ucheki mpakanni wa Bohemia.

Jina latokana na madini yaliyochimbwa katika milima hii hasa fedha kuanzia zama za shaba. Wakati wa karne za kati eneo hili ilikuwa chanzo muhimu cha fedha na pesa ya "Taler" (iliyoitwa "dollar" kwa Kiingereza) ilianzishwa hapa. Tangu karne ya 19 umuhimu wa mogodi imeendelea kupungua.

Milima ya juu ni Klínovec (jer.: Keilberg) yenye kimo cha mita 1,244 na Fichtelberg yenye kimo cha mita 1,215.