Nenda kwa yaliyomo

Emilio Bonifácio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bonifácio akiwa Chicago White Sox mnamo 2015
Bonifácio akiwa Chicago White Sox mnamo 2015

Emilio José Bonifácio Del Rosario (alizaliwa Aprili 23, 1985)[1] ni mchezaji wa baseball wa Jamhuri ya Dominikana ambaye kwa sasa ni mchezaji huru. Aliwahi kuchezea ligi ya MLB na timu za Arizona Diamondbacks, Florida/Miami Marlins, Toronto Blue Jays, Kansas City Royals, Chicago Cubs, Chicago White Sox, Atlanta Braves na Washington Nationals.

Awali alicheza kama baseman wa pili na baadaye alikuwa kiungo wa kati kipindi chote cha maisha yake ya kazi[2].

  1. "Emilio Bonifácio Stats, Fantasy & News". MLB.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-12-02.
  2. "Emilio Bonifacio Stats". Baseball-Reference.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2021-12-02.