Elizabeth Gitau
Elizabeth Gitau, pia anajulikana kama Elizabeth Gitau-Maina (amezaliwa takriban 1988), ni daktari wa tiba na mtendaji wa shirika kutoka Kenya. Kwa sasa, anahudumu kama Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Madaktari wa Tiba Kenya (Kenya Medical Association), shirika la kitaifa linalolenga kutetea na kuhifadhi maslahi ya madaktari wa tiba wanaofanya kazi nchini.[1]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Baada ya kuhitimu kutoka shule ya udaktari na kukamilisha mafunzo ya lazima kwa vitendo, Elizabeth Gitau alifanya kazi kama Afisa wa Matibabu katika Hospitali ya Kaunti ya Muranga kwa karibu miaka miwili hadi Desemba 2014.
Kufikia Aprili 2019, Gitau alikuwa mhadhiri mwandamizi katika Chuo cha Mafunzo ya Matibabu Kenya (Kenya Medical Training College), chuo kinachotoa mafunzo ya maafisa wa kliniki (zamani wasaidizi wa matibabu) katika ngazi ya diploma, kilichopo kwenye kampasi mjini Thika.[2]
Akiwa Afisa Mtendaji Mkuu mpya wa Chama cha Madaktari wa Tiba Kenya (Kenya Medical Association)[3], alichukua nafasi ya Stellah Wairimu Bosire-Otieno, ambaye aliongoza chama hicho kutoka 2017 hadi 2019. Hapo awali, Gitau aliwahi kuwa mweka hazina wa tawi la Kaunti ya Nairobi la Chama cha Madaktari wa Tiba Kenya.
Mnamo Machi 2021, wakati wa janga la COVID-19, Gitau aliikosoa Kenya kwa kupatia kipaumbele chanjo kwa wanadiplomasia badala ya wahudumu wa afya na wazee.[4]
Mnamo Machi 2023, Dkt. Elizabeth Gitau aliteuliwa kuwa mwanachama wa bodi ya Baraza la Madaktari wa Tiba na Madaktari wa Meno Kenya (Kenya Medical Practitioners and Dentists Council - KMPDC).[5] Pia ni mwanachama na mratibu wa Mtandao wa Madaktari Vijana (Young Doctors Network).[6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Stay up to date on the editors' picks of the week (2020-12-09). "Doctors' board picks first woman chair". Business Daily (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-12-22.
{{cite web}}
:|author=
has generic name (help) - ↑ "Dr. Elizabeth Gitau Maina – Kenya Medical Practitioners and Dentists Council". kmpdc.go.ke. Iliwekwa mnamo 2024-12-22.
- ↑ "HOME". web.archive.org. 2019-04-11. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-04-11. Iliwekwa mnamo 2024-12-22.
- ↑ "Local doctors angry as Kenya offers COVID vaccines to diplomats". Al Jazeera (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-12-22.
- ↑ "New KMPDC board members assume office, challenged to uphold professional ethics". The Star (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-12-22.
- ↑ "Dr. Elizabeth Gitau-Maina". Issuu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-12-22.