Nenda kwa yaliyomo

Donalda Ammons

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Donalda Kay Ammons (alizaliwa 15 Mei 1993) ni mwalimu na mwandishi nchini Marekani. Alihudumu kama mwalimu katika shule kadhaa za viziwi nchini Marekani. Pia, Ammons alikuwa Rais wa zamani wa Comite International des Sports des Sourds (CISS) kuanzia 2003 hadi 2009.[1]

Ammons alizaliwa Mei 15, 1953, na kukulia katika familia ya viziwi iliyopo Washington D.C. Alihitimu katika Shule ya Viziwi ya Maryland na baadaye akawa anafundisha katika shule hiyo kwa miaka mitatu. Mnamo 1970, alijiunga na elimu ya juu katika Chuo Kikuu cha Gallaudet na kuhitimu BA (Shahada Awali ya Sanaa) katika Falsafa ya Jamii.[2]

Mnamo 1996, alitunukiwa Uprofesa kama Profesa wa mwaka wa Gallaudet.[3]

Huduma kwa viziwi

[hariri | hariri chanzo]

Akiwa kama mtu mwenye ulemavu wa kutokusikia, Ammons amekuwa mwalimu katika shule nyingi za viziwi. Mnamo 1977, alifundisha katika Shule ya Viziwi ya Maryland kwa miaka mitatu. Pia, alifundisha Kihispania katika idara ya lugha za kigeni na fasihi katika Chuo Kikuu cha Gallaudet, ni Chuo kinachohudumia (kulea) viziwi.[4][5][6]

Olimpiki ya viziwi

[hariri | hariri chanzo]

Ammons alikuwa Mwanachama wa Comite International des Sports des Sourds tangu 1997. Aliteuliwa kama Katibu Mkuu wa nne wa CISS, mnamo 1997 na alikuwa mwanamke wa kwanza kushikilia wadhifa huo.[7][8] Ammons alikuwa Rais wa 7 wa CISS mnamo 2003, akihudumu kama Rais wa Mpito hadi 2005 kuafuatia cha rais aliyekuwapo, John Michael Lovett. Ammons alichaguliwa rasmi kama rais wa awamu ya 7 wa Kamati mnamo 2005 na kuwa mwanamke wa kwanza aliyechaguliwa kuwa Rais wa CISS. Alihudumu kama Rais wa ICSD kuanzia 2003 hadi 2009.[9]

Tuzo na heshima

[hariri | hariri chanzo]

. Profesa wa Mwaka wa Gallaudet (1996)

. Profesa wa Emirita katika Chuo Kikuu cha Gallaudet[10]

. Tuzo ya Edward Miner Gallaudet (1992)

  1. "ICSD | Deaflympics". www.deaflympics.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-10-25. Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  2. Administrator. "DDW Board Profiles - Donalda Ammons, Ph.D." www.discoveringdeafworlds.org (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  3. "President Ammons Presents at 2006 World Conference on Women and Sport in Kumamoto, Japan", ciss.org. (en) 
  4. "Deaf Women United". Deaf Women United. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-07. Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  5. University, Gallaudet. "Gallaudet Video Presents Links with Dr. Donalda Ammons - Gallaudet University". videocatalog.gallaudet.edu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  6. "News | Deaflympics". www.deaflympics.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-07. Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  7. "ICSD | Deaflympics". www.deaflympics.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-07. Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  8. "History – Historia", PANAMDES, 2012-07-11. (en-US) 
  9. "42nd Congress of the ICSD | Deaflympics". www.deaflympics.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-11-30. Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
  10. "Donalda Ammons at Gallaudet University - RateMyProfessors.com". www.ratemyprofessors.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-07. Iliwekwa mnamo 2017-11-01.
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Donalda Ammons kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.