Die Welt

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Die Welt
Jina la gazeti Die Welt
Aina ya gazeti Gazeti la kila siku
Lilianzishwa 2 Aprili 1946
Eneo la kuchapishwa *.Berlin
*.Hamburg
*.Bremen
Nchi Ujerumani
Mwanzilishi majeshi ya Uingereza
Mhariri Thomas Schmid
Mmiliki Axel Springer AG
Makao Makuu ya kampuni Berlin
Machapisho husika *. Welt am Sonntag (jarida la Jumapili)
*. Welt Kompakt
Tovuti http://www.welt.de

Die Welt ni gazeti la kila siku la Ujerumani. Gazeti hili huchapishwa na kampuni ya Axel Springer AG.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Lilianzishwa katika mji wa Hamburg katika mwaka wa 1946 na majeshi ya Uingereza yaliyokuwa huko. Walitaka kuchapisha gazeti la hali ya juu linalofanana na lile la The Times la Uingereza. Hapo mwanzoni, lilichapisha habari kutokana maoni ya Uingereza lakini kutoka mwaka wa 1947 lilianza kuwa na sera ya kuchapisha makala mawili kuhusu masuala muhimu , moja la maoni ya Kiingereza na moja la maoni ya Kijerumani. Katika upeo wake, gazeti hilo lilikuwa na usambazaji wa nakala takriban milioni moja.

Jarida hili, hivi sasa, huchukua mfumo wa "gazeti huria la jiji" katika uhariri wake lakini Die Welt husemekana na wengi kuwa gazeti la kihafidhina.

Usambazaji wa wastani wa gazeti la Die Welt ni nakala 209,000 na gazeti hili hupatikana katika nchi 130. Matoleo ya kila siku ya maeneo mbalimbali hupatikana Berlin na Hamburg. Katika mwaka wa 2002, gazeti hili lilijaribu kuchapisha toleo la Kibavaria. Toleo dogo la kila siku hupatikana katika mji wa Bremen. Ofisi kuu za uhariri zinapatikana jijini Berlin, zikiwa pamoja na za Berliner Morgenpost.

Die welt ndilo gazeti maarufu kabisa katika magazeti ya kundi la Axel Springer la uchapishaji. Magazeti shindani yake ni Frankfurter Allgemeine Zeitung, Süddeutsche Zeitung na Frankfurter Rundschau Katika sekta ya kifedha , limekuwa likileta hasara kwa miaka mingi lakini bado huchapishwa.

Die Welt ni mojawapo wa waanzilishi wa European Dallies Alliance na huwa na uhusiano mzuri na magazeti ya kuchapishwa kila siku ya nchi nyingine kama magazeti ya Daily Telegraph (Uingereza), Le Figaro (Ufaransa) na ABC (Uhispania).

Hivi sasa gazeti hili huchapisha toleo dogo la gazeti hili linaloitwa Welt Kompakt, toleo la kurasa 32 lililofupisha gazeti lenyewe. Welt Kompakt huchapishwa kwa mitindo mipya inayolenga kuvutia vijana. Gazeti hili halichapishwi Jumapili lakini jarida jingine la Welt am Sonntag huchapishwa siku hiyo.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^ Patricia Meehan, A Strange Enemy People: Germans under the British 1945–50. London: Peter Owen, 2001, pp. 176–9. ISBN 0720611156.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]