Nenda kwa yaliyomo

Delavirdine

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Delavirdine (DLV), inayouzwa kwa jina la chapa Rescriptor, ni dawa inayotumika kufubaza Virusi vya UKIMWI.[1] Inatumika pamoja na dawa nyingine za VVU; ingawa sio tiba inayopendekezwa.[1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo, mara tatu kwa siku.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na uchovu, kizunguzungu, maumivu ya kichwa na upele.[2] Dalili zake nyingine zinaweza kujumuisha ugonjwa wa Stevens-Johnson, unene wa kupindukia na ugonjwa wa kurejesha kingamwili.[1] Usalama wa matumizi yake katika ujauzito hauko wazi.[1] Dawa hii ni kizuizi kisicho na nucleoside reverse transcriptase (NNRTI).[1]

Delavirdine iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 1997 [1] lakini ilikomeshwa nchini Marekani kufikia mwaka wa 2021.[1] Dawa hii haitumiki kwa kawaida.[2]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 1.6 1.7 "Delavirdine Mesylate Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 Mei 2016. Iliwekwa mnamo 23 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 "Delavirdine". LiverTox: Clinical and Research Information on Drug-Induced Liver Injury. National Institute of Diabetes and Digestive and Kidney Diseases. 2012. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 6 Mei 2021. Iliwekwa mnamo 23 Desemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Delavirdine kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.