Nenda kwa yaliyomo

David Rudisha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
David Rudisha akiwa Beijing mwaka 2015

Daudi Lekuta Rudisha (aliyezaliwa 17 Desemba 1988) ni Mkenya mkimbiaji wa umbali wa kati.Yeye ndiye anashikilia rekodi ya Olimpiki na ya dunia ya mbio za mita 800.[1]

Maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa mjini Kilgoris, Wilaya ya Trans Mara nchini Kenya.Rudisha alienda shule ya St Patrick,shule ya upili ya Kimuron huko Iten, Wilaya ya Keiyo, ambayo inajulikana kwa kuwalea wakimbiaji kadhaa ikiwa ni pamoja na Wilson Kipketer aliyekuwa ameshikilia rekodi ya mbio za mita 800m kwa miaka kadhaa kabla ya Rudisha kujiunga na shule hiyo. Mnamo Aprili 2005 Japheth Kimutai alipendekeza Rudisha kwa James Templeton, na Rudisha akajiunga na kundi la wakimbiaji linalosimamiwa na Templeton.[2]

Virejeleo

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Men's 800 Metres All-Time List". International Association of Athletics Federations. Iliwekwa mnamo 11 Agosti 2012. {{cite web}}: Text ",AAF.org" ignored (help)
  2. IAAF, 13 Septemba 2009: Rudisha: Following in the footsteps of Konchellah and Kipketer?. Retrieved 23 Agosti 2010.