Daudi Kabaka
Daudi Kabaka (1939-2001) ni mwimbaji mzaliwa wa Kenya.
Aina ya muziki anayojulikana nayo inaitwa 'Benga', mtindo maarufu sana katika Afrika Mashariki. Nyimbo zake bora zinazojulikana ni pamoja na "African Twist", "Harambee Harambee" na "Western Shilo".
Wimbo wake wa "Helule Helule" uliangaziwa na The Tremeloes na ulitamba sana nchini Uingereza.
Daudi Kabaka pia anajulikana nchini Kenya kwa wimbo wake "Harambee Harambee" ambao kwa kiasi kikubwa huonyesha matumainio ya Wakenya baada ya ukolini ya kuazimi kujenga taifa la Kenya upya.
Alishirikiana na John Nzenze kwenye nyimbo tatu: Masista ,Bachelor Boy na Nyumba za Tumbaku . Nyimbo hizi zilitolewa na Jambo Records na zikavuma sana[1] Kabaka alitoa katika albamu ya "Pesa Maradhi Ya Moyo" na Maroon Commandos mwaka wa 1986 [2]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Daily Nation, 14 Juni 2009: At 70, Nzenze still holds on to his guitar
- ↑ Muzikifan.com: DISCOGRAPHY OF EAST AFRICAN MUSIC Part 2: POLYGRAM (Kenya)
Kigezo:Mkala ya mbegu ya uhai ya Kenya Kigezo:Mkala ya mbegu ya waimbaji wa Afrika