Clube de Regatas do Flamengo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nembo ya timu ya flamengo
Makala hii kuhusu "Clube de Regatas do Flamengo" ni fupi mno. Inahitaji kupanuliwa mapema.

Clube de Regatas do Flamengo ni klabu ya kandanda yenye makao yake katika mji mkuu wa Rio de Janeiro nchini Brazil.

Flamengo hii ilianzishwa 1 Septemba 1895,na ni moja kati ya timu kubwa nchini brazil yenye mashabiki wengi karibu milioni 39 kutokana na mafanikio ya yake.

Kiasili klabu ya flamengo huvaa jezi zenye rangi nyekundu na nyeusi,bukta nyeupe na soksi nyeusi. Na pia hutumia uwanja wa maracana kama uwanja wa nyumbani wenye uwezo wa kubeba karibu watu 78,800 na ni uwanja mkubwa kuliko viwanja vyote nchini brazil. Kwa sasa flamengo inatumia uwanja wake mdogo kwa kipindi cha mpito unaoitwa Ilha Do Urubu.

Moja ya kitu muhimu ambacho klabu ya flamengo wanajivunia licha kuchukua makombe mengi ni moja ya timu kati ya tano ambazo hazijawahi kushuka daraja,ni pamoja na Santos, Sao Paolo , Chapecoense, Cruzeiro Na Flamengo yenyewe. Wapinzani Wakubwa Wa Timu Ya Flamengo Ni Fluminese, Botafogo na Vasco Da Gama.