Nenda kwa yaliyomo

Clitoraid

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Clitoraid Adopt a Clitoris event in South Korea, July 2006

Clitoraid ni mradi usio na faida kibiashara ambao ulianzishwa na harakati za Raëlism/Raelian ili kupinga ukeketaji.

Mradi huu ulianzishwa kati ya mwaka 2005[1] au 2006.[2] Harakati hizi za Raeliani huona kwamba kuridhika kingono ni jambo chanya na Clitoraid walifadhili wanawake wa Afrika na walitaka kujenga hospitali huko Burkina Faso[3] ambapo wangepokea maelekezo ya awali kuhusu punyeto.[4] Clitoraid walipata ufadhili wa mradi huu wa kupinga ukeketaji,[5] ambao ulitangazwa katika AVN Adult Entertainment Expo huko Las Vegas.[1][6]

Mwaka 2010, katika kumtia moyo mtaalamu wa masuala ya mapenzi Betty Dodson, duka la San Fransisko linalosambaza vifaa vya kuchochea ashiki waliahidi kutoa msaada wa fedha kwa Clitoraid ikiwa ni pamoja na kuwaomba wateja kuchangia; kampuni iliiondoa ofa hiyo baada ya kupata upinzani kwamba juhudi hazikutumika ipaswavyo, hasa kutoka kwa Wanjiru Kamau-Rutenberg, profesa wa siasa katika chuo kikuu cha San Francisco.[2][7]

Mwaka 2013, Clitoraid walipendekeza wiki ya Mei 6–12 kama "Wiki ya kimataifa ya kutoa elimu dhidi ya ukeketaji".[8]

Kufunguliwa kwa Hospitali ya Kamkaso mwaka 2014 ama Hospitali ya Raha huko Bobo-Dioulasso kulicheleweshwa na wizara ya afya ya Burkina Faso.[9] Clitoraid walililaumu Kanisa Katoliki kwa hilo.[10]

Mwaka 2015, katika kujibu mzozo dhidi ya kutahiriwa kwa mvulana wa miaka 4 wa Marekani, Clitoraid walitoa taarifa kwa vyombo vya habari wakiwa upande wa mama ambaye hakutaka mtoto wake atahiriwe. Pia waliwataka Umoja wa mataifa kupiga marufuku jambo hili: "Kujeruhi mwili ni kunyume na haki ya msingi kwa watoto wote, na hatuwezi kuelewa kwamba nchi inayojiita imestaarabika kama Marekani kuhalalisha kutahiriwa kwa watoto wake wa kiume!"[11]

  1. 1.0 1.1 "Clitoraid at the AVN Porn Convention in Las Vegas". Raelia News. 23 Januari 2007.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. 2.0 2.1 Blue, Violet (19 Mei 2010). "Good Vibrations And The Clitoris Saving Alien Cult". SF Appeal. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-06-07. Iliwekwa mnamo 2021-07-22.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Deploring death of teenage Kenyan FGM Victim", Newstime Africa, 23 April 2014. Retrieved on 2021-07-22. Archived from the original on 2017-03-06. 
  4. "'Pleasure hospital' in Burkina Faso to restore clitoral functioning for women mutilated in childhood". Raelia News. 16 Mei 2007. Iliwekwa mnamo 6 Mei 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. "Adopt A Clitoris". Raelia News. 15 Mei 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. Fretwell, Alonzo (31 Januari 2011). "Clitoraid at 2011 Adult Entertainment Expo in Las Vegas". Raelia News.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Millner, Caille. "Wrong approach to ending genital mutilation", 14 April 2010. 
  8. Moye, David. "'International Clitoris Awareness Week' Takes Place May 6-12 (NSFW)", The Huffington Post, 5 February 2013. Retrieved on 24 April 2014. 
  9. Lloyd-Roberts, Sue. "FGM, Clitoraid and The Pleasure Hospital: US sect the Raëlians’ quest to ‘restore’ women scarred by female genital mutilation in Burkina Faso", 16 March 2014. Retrieved on 2021-07-22. Archived from the original on 2015-09-25. 
  10. Clitoraid Inc. "Catholic Church prevents March 7 opening of Clitoraid's 'Pleasure Hospital' - Clitoraid.org Restoring a Sense of Pleasure and Dignity". clitoraid.org. Iliwekwa mnamo 21 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  11. "Press release: "Clitoraid supports Florida mother who faces prison for refusing to have her little boy Genitally Mutilated. Clitoraid asks U.N. to ban childhood Genital Mutilation worldwide for both genders"". Clitoraid. Iliwekwa mnamo 6 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)