Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Koitalel Arap Samoei

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Chuo Kikuu cha Koitalel Arap Samoei ni chuo kikuu kilichopo Nandi katika nchi ya Kenya[1], kilifunguliwa mnamo mwaka2015.[2]

Serikali ya Nandi ilikubaliana na Chuo Kikuu cha Nairobi kujenga chuo kikuu kipya kitakachopewa jina la kiongozi mashuhuri,Koitalel Samoei,aliuawa mwaka 1905 na wakoloni.

Kuanzia 2014 chuo kikuu kilikuwa katika mchakato wa kudahili wanafunzi katika Chuo cha Chuo Kikuu cha Koitalel Arap Samoei kwa kozi za kuanza Januari 2015.

Chuo Kikuu cha Nairobi kimetenga bajeti ya Bilioni 2 kutoka kwa Serikalini kwaajili ya ujenzi huo kulingana na tovati ya Serikali ya Kaunti ya Nandi.

Programu za masomo zitakazotolewa katika chuo kikuu ni Sheria, Elimu na Usimamizi wa Biashara.Chuo kikuu kitatumia miundo iliyopo ya Shule ya Upili ya Samoei. Tume ya Elimu ya Chuo Kikuu nchini Kenya ilisema kuwa imeridhika kwamba ardhi inayopatikana shuleni ni zaidi ya ekari 100 na kwa hivyo inatosha kwa upanuzi. Kuanzia mwaka wa 2018 ujenzi unaendelea.

  1. "Nandi County To Spend 2B To Build Koitalel University - Citizen News". web.archive.org. 2014-12-23. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-12-23. Iliwekwa mnamo 2021-06-19.
  2. "Nandi County To Spend 2B To Build Koitalel University". Citizentv.co.ke (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2021-06-19.
Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chuo Kikuu cha Koitalel Arap Samoei kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.