Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Howard

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Muhuri Rasmi wa Chuo Kikuu Cha Howard

Chuo Kikuu cha Howard ni shule binafsi katika mji wa Washington D.C. nchi ya Marekani. Ni “chuo kikuu cha watu Weusi” au HBCU[1]. Pia ni chuo kikuu chenye cheo cha “R2” ikimaanisha kwamba utafiti mwingi unafayika huko.[2]

Chuo Kikuu cha Howard ilifunguliwa katika mwezi wa tatu, mwaka 1867, baada ya vitu vya wenyewe kwa wenyewe Marekani.

Maisha wa Wanafunzi

[hariri | hariri chanzo]

Wanafunzi wanaita shule hiyo Makka (au “The Mecca” kwa Kiingereza), kwa sabubu ni mahali muhimu kwa utamaduni ya watu Wafrika na Weusi. 86% ya wanafunzi ni Waamerika wa Kiafrika au Weusi.[3]

Chuo kikuu cha Howard ni mahali kwa uumbaji wa Baraza la Kitaifa la Pan-Hellenic (au National Pan-Hellenic Council kwa Kiingereza). Iliundwa ili wanafunzi Weusi wawe na udugu na uchawi ambao wanaweza kujiunga nao.

Programu za masomo

[hariri | hariri chanzo]

Chuo kikuu cha Howard kuna chuo kumi na tatu ndani ya chuo kikuu. Kuna Chuo cha Uhandisi na Usanifu Majengo, Chuo cha Uguzi na Sayansi Shirikishi za Afya, Chuo cha Famasia, Chuo cha Sanaa na Sayansi, Chuo cha Sanaa Nzuri ya Chadwick Boseman, Chuo cha Utaalamu wa Meno, Shule ya Biashara, Shule ya Mawasiliano ya Cathy Hughes,  Chuo cha Tiba, Shule ya Sheria, Shule ya Kati ya Hisabiti na Sayansi, Shule ya Uungu, Shule ya Elimu, na Shule ya Kazi ya Jamii. Kuna shahada ya kwanza, shahada ya pili, na shahada ya tatukwa programu wengi.[4]

Programu ya Masomo ya Kiafrika

[hariri | hariri chanzo]
Mtazamo wa Chuo Kikuu cha Howard

Chuo Kikuu cha Howard kinajulikana sana kwa kuwa programu ya masomo ya Kiafrika nzuri sana. Programu ya Masomo wa Kiafrika katika Chuo Kikuu cha Howard ina programu ya lugha ya Kiafrika ndani ya programu hii. Katika Chuo Kikuu cha Howard walimu wanafundisha lugha wengi kama Kiamhara, Kiarabu, Kisomali, Kiswahili, Kiyoruba, Kiwolof, na Kizulu. Kituo cha Masomo ya Kiafrika ya chuo kikuuni kuna utaalamu wengi kwa masomo wa lugha ya Afrika.

Huru ya kituo cha masomo ya Kiafrika kuna kituo cha utafiti cha Moorland-Spingarn. Ni kituo cha utafiti ambacho kinavutiwa na hifadhi ya hati na kulinda kwa hati kuhusu utamaduni na historia ya watu Wafrika katika Afrika, katika Amerika ya Kaskazini na Amerika Kusini, katika visiwa vya Caribbean, na sehemu mbalimbali za dunia. [5]

Wanafunzi Maarufu wa Zamani

[hariri | hariri chanzo]
Foto ya Chadwick Boseman

Chuo kikuu cha Howard ina wanafunzi wengi wa zamani ambao wamekuwa watu maarufu. Baadhi ya mifano ya wanasiasa maarufu ni pamoja na Makaumu wa Rais Marekani Kamala Harris, Jaji wa Makamu ya Juu Thurgood Marshall, Meya Ras baraka wa jiji la Newark jimbo la New Jersey. Pia kuna waigizaji maarufu sana kama Chadwick Boseman, Taraji P. Henson, Anthony Anderson, na Nick Cannon.

  1. "Howard University and Lowe To Develop Mixed-Use Building Near University Campus". The Dig at Howard University (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
  2. "Carnegie Classifications | Home Page". web.archive.org. 2022-05-27. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2022-05-27. Iliwekwa mnamo 2024-04-24. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help)
  3. "Howard University (HU, HU) Introduction and Academics - Washington, DC". www.stateuniversity.com. Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
  4. "Fields of Study | Howard University". howard.edu (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2024-04-24.
  5. "History". web.archive.org. 2007-11-06. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2007-11-06. Iliwekwa mnamo 2024-04-24. {{cite web}}: Cite has empty unknown parameter: |dead-url= (help)