Chris Tonietto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Christine Nogueira do Reis Tonietto, anajulikana zaidi kama Chris Tonietto alizaliwa mnamo mwezi wa tano,tarehe14, 1991, ni mwanasheria na mwanasiasa Mbrazil aliyejiunga na Chama cha Liberal Part(PL) na kwa sasa ni mbunge huko jijini Rio de Janeiro.

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Christine Nogueira dos Reis Tonietto alizaliwa katika mji wa Rio de Janeiro tarehe 14 Mei 1991 na alihitimu shahada ya sheria katika chuo kikuu cha Fluminense federal university (UFF) mnamo mwaka 2016.

Kama mwanasheria Mkatoliki na mwanachama wa kituo cha utamaduni Centro Dom Bosco, mnamo mwaka 2017 alijihusiha katika kikundi cha maigizo kwenye kipindi cha komedi kwenye mtandao wa kijamii wa Porta dos Fundos, kwa sababu ya video yake inayodhihaki mbingu katika Ukatoliki. Mchakato huo ulifutwa bila kuchunguzwa kwa msingi mwaka uliofuata, kutokana na kutolipwa kwa gharama za mchakato. Katika uchaguzi wa Oktoba 7, 2018, Tonietto alichaguliwa kuwa mbunge wa shirikisho wa Chama cha Kiliberali cha Jamii na Rio de Janeiro kwenye Bunge la kitaifa la 56 na kupata kura 38,129 (0.50% ya kura halali).Badae alichaguliwa tena kwa muhula wa pili mnamo mwaka 2022 na kura 52,583 (0.61% ya kura halali).

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Chris Tonietto kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.