Cheluchi Onyemelukwe
Cheluchi Onyemelukwe ni muandishi wa vitabu na mtaaluma mwenye uraia wa Nigeria pamoja na Kanada.
Anajulikana kwa riwaya yenye maudhui ya familia aliyoiandika mwaka 2019 iitwayo The Son Of The House iliomfanya ashinde tuzo ya Nigeria Prize of Literature mwaka 2021. Vilevile ni Profesa wa Sheria katika chuo cha Babcock University ambapo mwanzoni alikuwa profesa msaidizi. Mnamo mwaka 2019 alishinda kitabu bora cha kufikirika kimataifa katika Sharjah International Book Fair. Mwaka 2021 alishinda tuzo nyingine katika SpriNG Women authors prize. Riwaya yake pia ilipendekezwakatika Giller Prize mwaka 2021.[1]
Maisha ya Awali na Kazi
[hariri | hariri chanzo]Onyemelukwe ni raia wa Naijeria.[2] Alisoma katika chuo cha Dalhousie huko Nova Scotia, Kanada akichukua shahada ya udaktari katika masual ya Sayansi ya Mahakama na vilevile alisoma University Of Nigeria alipopata shahada yake ya kwanza ya Sheria.[3]
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Damiete Braide. "BREAKING: Cheluchi Onyemelukwe-Onuobia wins Nigeria Prize for Literature 2021", October 30, 2021.
- ↑ Chukwuebuka Ibeh. "Cheluchi Onyemelukwe-Onubia wins inaugural SprinNG women authors prize". Brittle Paper. Iliwekwa mnamo Septemba 8, 2021.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Adina Bresge (Oktoba 5, 2021). "Two-time runner-up Miriam Toews among authors on Giller Prize shortlist". The Globe and Mail.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Cheluchi Onyemelukwe kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |