Catherine Zeta Jones
Catherine Zeta-Jones (amezaliwa tar. 25 Septemba 1969) ni mshindi wa tuzo ya Academy-mwigizaji bora filamu wa Kiwelisi anayevuma na kuishi nchini Marekani.
Zeta alianza shughuli za uigiza tangu akiwa mdogo. Baada ya hapo, akawa anaigiza katika sehemu nyingi ndogo-ndogo za filamu na tamthilia za Kiingereza na Kiamerika.
Ameanza kuwa miongoni mwa waigizaji walio maarufu baada ya kujiingiza katika uchezaji wa filamu za Hollywood, moja kati ya filamu alizocheza ni kama ifuatavyo: The Phantom, The Mask of Zorro, na Entrapment iliyocheezwa kunako miaka ya 1990.
Zeta pia aliwahi kushinda tuzo ya Academy kama mwigiza msaidizi-bora wa katika filamu ya Chicago iliyochezwa mwaka 2002 na humo aliigiza kama Velma Kelly. Ni mwanamama wa kwanza wa Kiwelisi-pekee aliyewahi kushinda tuzo hiyo. Zeta-Jones ameolewa na bwana Michael Douglas, ambaye wanafanana tarehe za kuzaliwa. Kwa pamoja wamezaa watoto wawili - Dylan na Carys.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Catherine Zeta-Jones at the Internet Movie Database
- Catherine Zeta Jones katika People.com
- Catherine Zeta-Jones katika Movies.com