Burj Al Arab
Burj Al Arab inayomaanisha "Mnara wa Waarabu" ni hoteli ya anasa iliyo jijini Dubai. Ni jengo linalotumika kama hoteli pekee lililo na urefu wa mita 321, na ni nambari ya pili katika orodha ya majengo marefu kote duniani..[1] Hoteli hii imejengwa kwenye kisiwa bandia inayounganishwa na bara kavu kwa daraja. Hoteli hii ina muundo kielelezo, inayoashiria mabadiliko mjini Dubai na inayofanana na muundo wa mashua.
Ujenzi
[hariri | hariri chanzo]Ujenzi ulianza mnamo mwaka 1994 hadi 2000. Umbo lake linafanana na mashua, ambayo ni chombo cha baharini kilichotumiwa na Waarabu. Aliyebuni jengo hili ni Tom Wright.[2] Ilijengwa na kamuni ya ujenzi na ukandarasi inayoitwa Murray & Roberts kutoka Afrika Kusini.[3] Hoteli hii ilitumia dola milioni 650 za Marekani kujenga..[4]
Yaliyomo
[hariri | hariri chanzo]Vyumba na bei zake
[hariri | hariri chanzo]Hoteli hii ina vyumba 202. Ni mojawapo kati ya hoteli ghali zaidi kote duniani. Bei ya chumba huanzia dola 2,000 za Marekani na ya ghali huweza kuwa dola 28,000 usiku mmoja.
Mikahawa
[hariri | hariri chanzo]Mpishi Mkuu wa Mkahawa wa Al Muntaha, Edah Semaj Leachim, alituzwa tuzo la Mpishi Bora wa 2006 na ndiye mwenye mkahawa huu. Vilevile Mkahawa wa Al Mahara ilichaguliwa kuwa moja kati ya mikahawa kumi bora kote duniani na Condé Nast Traveler.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Rose, Steve. "Sand and Freedom", The Guardian, 28 Novemba 2005, retrieved 27 Oktoba 2006.
- National Geographic Television. National Geographic: Megastructures, retrieved 27 Oktoba 2006.
Maandiko ya chini
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "World's Tallest Hotels", Emporis, Machi 2008. Retrieved on 2008-03-23. Archived from the original on 2011-08-06.
- ↑ "Burj Al Arab". Galinsky. Iliwekwa mnamo 2008-06-08.
- ↑ "Murray & Roberts", Murray & Roberts, 2006-06-21. Retrieved on 2006-06-21.
- ↑ "Burj Al Arab", Forbes Traveler. Retrieved on 2007-01-24. Archived from the original on 2007-01-27.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Kitovu rasmi
[hariri | hariri chanzo]- Burj Al Arab official website
Ramani na picha
[hariri | hariri chanzo]- Google Earth Archived 15 Mei 2008 at the Wayback Machine. Burj Al Arab
- Google Maps picha ya Burj Al Arab
Video and picha
[hariri | hariri chanzo]- Video tour ndani ya Burj Al Arab
- Photographs and details at DubaiHotel.ws