Volta Nyeusi

Volta Nyeusi (pia: Mouhoun au Volta Noire kwa [[Kifaransa])[1]) ni mojawapo ya ya mito mitatu mikuu inayounda mfumo wa Mto Volta, mingine ikiwa Volta Nyeupe na Volta Nyekundu.[2]. Ni mto unaopitia Burkina Faso kwa takribani kilomita 1,352 (mile 840) hadi Volta Nyeupe huko Dagbon, Ghana, sehemu ya juu ya Ziwa Volta. [3]
Chanzo chake kiko katika mkoa wa Cascades wa Burkina Faso, karibu na Mlima Tenakourou, sehemu ya juu kabisa ya nchi. Mto huo kwa chini zaidi unakuwa sehemu ya mpaka kati ya Ghana na Burkina Faso, na baadaye kati ya Cote d'Ivoire na Ghana. Ndani ya Ghana, inaunda mpaka kati ya mikoa ya Savannah na Bono. [4][3] Bwawa la Bui, mtambo wa kuzalisha Umememaji, umejengwa kwenye mto, kusini kidogo tu mwa Mbuga ya Taifa ya Bui, ambapo mto huo hupita, na kuigawa katika sehemu mbili.[5]unaigawanya. [3][6]
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Amisigo, Barnabas Akurigo (2005). Modelling Riverflow in the Volta Basin of West Africa: A Data-driven Framework (kwa Kiingereza). Cuvillier Verlag. ISBN 978-3-86537-701-2.
- ↑ "Upper Volta (Burkina Faso, 1959-1984)". www.fotw.info. Iliwekwa mnamo 2026-06-14.
- 1 2 3 "Ghana - Rivers and Lakes". www.countrystudies.us. Iliwekwa mnamo 2017-08-17.
- ↑ "CONFIRMED: Results of the 2018 Referendum on new regions". Graphic Online (kwa Kiingereza (Uingereza)). Iliwekwa mnamo 2020-08-18.
- ↑ "Ghana Wildlife, Wildlife Division Ghana, Wildlife in Ghana, National Parks in Ghana, ghana wildlife sanctuary, List of Parks in Ghan". ghanawildlife.org. Iliwekwa mnamo 2026-06-14.
- ↑ "Bui National Park". Ghana Wildlife Division. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 23 Aprili 2018.
{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Volta Nyeusi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |