Nenda kwa yaliyomo

Biladol Orb Awtani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Bilad Alorib Awutani (Kiarabu: بلاد العرب أوطاني) au Nchi za Kiarabu ni taifa langu ni wimbo wa kitaifa wa (Pan-Arabism) ambao husomwa kwa lugha ya Kiarabu. Unatambuliwa isivyo rasmi kama wimbo wa taifa wa Ulimwengu wa Kiarabu, na umeandikwa na (Fakhri Al-Baroodi) na kutungwa na ndugu wa (Folayfel).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Wimbo huu ni wimbo wa Kiarabu unaojulikana sana, unaoita Umoja wa Waarabu, na unazingatia Umoja, Elimu, na kutunza mila na Utamaduni wa Kiarabu. Kufuatia Mapinduzi ya Kiarabu, wimbo huo ulitumiwa sana kama Wimbo wa Taifa wa Kiarabu usio rasmi katika matukio kadhaa, ikiwa ni pamoja na Michezo ya (Pan Arab) ya 2011.