Bikari

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa kundinyota angalia Bikari (kundinyota)

Kuchora duara kwa kutumia bikari

Bikari (ing.: pair of compasses) ni zana ya kazi kwa wachoraji na wanahisabati kwa kuchora duara. Pamoja na ramani inasaidia pia kupima umbali kwa hiyo ni pia zana ya ubaharia.

Bikari hutengenezwa kwa metali fulani au plastiki, kama ni kubwa kuna pia mifano ya ubao. Ina miguu miwili inayounganishwa kwa bawaba isiyocheza lakini inabana mikono kiasi isichezecheze kirahisi. Mkono wa kusimama huwa na ncha kali kama sindano, na mwingine unaishia kuwa kalamu au kuwa na kalamu iliyofungwa hapa.

Mkono unaoishia kwenye sindano unasimamishwa juu ya karatasi kwenye kitovu cha duara. Rediasi inawekwa kwa kufungua pembe kati ya mokono. Wakati bikari inazungushwa mguu mwenye kalamu inachora duara.