Benito Juárez
Mandhari
Benito Pablo Juárez García (21 Machi 1806 - 8 Julai 1872) alikuwa rais wa Meksiko mara tano (1858–1861 ), (1861–1865), (1865–1867), (1867–1871) na (1871–1872). Alizaliwa katika jamii ya Wazapoteki. Alipokuwa raisi wa Mexiko alipiga marufuku utumwa. Aliongoza nchi yake katika urekebishaji wa sheria nyingi. Hapo alitenganisha dola na athira kubwa ya Kanisa Katoliki akianzisha ndoa ya kiraia, uhuru kwa madhehebu na dini nyingine na kugawa ardhi kwa wakulima wadogo.
1861-8171 aliongoza upinzani wa Meksiko dhidi ya uvamizi wa Ufaransa na utawala wa Kaisari Maximilian I .